KAZI MAALUM: kuchambua makala kutoka vyanzo mbalimbali ili kupata suluhu ya changamoto zinazoikabili jamii hususani vijana. NDOTO: kuwa na jamii yenye utulivu wa kifikra, utulivu utakaoondoa; msongo wa mawazo, migogoro, vurugu, n.k. Kisha kuleta ustawi wa mtu mmoja mmoja, jamii, na Taifa zima kwa ujumla katika nyanja zote za maisha.
Sunday, December 23, 2012
JE NI WAKATI GANI WA KUNUNUA HISA WENYE MANUFAA ZAIDI KWA MWEKEZAJI?
Kwa Mwanahisa kujua hasa ni wakati gani wa kununua hisa, hiyo tayari ni sehemu ya uwekezaji katika Soko la hisa la Dar es salaakm. Lakini wawekezaji wengi wa ndani hawaoni fursa hii kwa kukosa au kutokuwa na taarifa/maarifa muhimu kuhusu uwekezaji kwenye hisa.
Moja ya wakati mzuri wa kuwekeza kwenye hisa ni pale ambapo kampuni inato hisa zake sokoni ili kuongheza mtaji wake (Initial Public Offers - IPO), wakati huo hisa huuzwa kwa bei ya chini na baada ya daftari la hisa kufungwa na kupelekwa kenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE) wawekezaji hao huziuza hisa hizo kwa bei ya juu na kupzta faida. Hii ni njia mojawapo ya kuopngeza faida kwa haraka, na hatari yha kupoteza thamani ya uwekezaji inakuiwa ndogo hasa pale wawekezaji (wanunuzi wa hisa) wanapokuwa wengi katika soko la hisa.
Licha yahiyo kuna njia nyingine ambazo zinarudisha faida nzuri kwenye uwekezaji wa hisa. Mojawapo ni pale ambapo bei ya hisa kwenye soko inakuiwa imeshuka au iko chini, ila ni muhimu kufanya utafiti au kufuatilia mahesabu ya kampuni unayotaka kuwekeza au kwa kutumia wataalamu wa masuala ya fedha (financial analysts). Bei ya hisa kupanda au kushuka katika soko, ni jambo la kawaida na inasababishwa na mambo mengi.
Mambo mawili makubwa ni kwamba, kampuni haifanyi vizuri na wawekezaji wake wameamua kuondoa mitaji yao kwenye hiyo kampuni na kuacha kuwekeza. Hii utaijua iwapo utakuwa unafuatilia kwa undani utendaji wa kampuni na siyo tu kuangalia bei ilioyoo sokoni. Jambo la pili ni kwamba, bei ya hisa inaendeshwa kutokana na nguvu ya soko inayoendeshwa na wanunuzi na wauzaji wa hisa. Hapa bei ya hisa inakuwa haiendani na utendaji wa kampuni. Utakuata kampuni inatengeneza faida kila mwaka na mahesabu yake yako wazi kuonyesha ufanisi wake , bado bei inakuwa chini. Huo ndio wakati mzuri wa kununua hisa kwa sababu pamoja na kwamba bei ya hisa za kampuni hiyo ziko chini ya bei iliyouzwa sokoni kwa mara ya kwanza, lakini bado kampuni inatengeneza faida. Hisa hizi zinakuwa ni nafuu na rahisi kulinganisha na thamani halisi ya hisa.
Ni muhimu sana kwa wawekezaji katika hisa kusoma kwa undani mahesabu na mwenendo wa kampuni wanayotaka kuwekeza kabla ya kufanya maamuzi ya kununua au kuuza hisa zo. Kwa upande mwingine kuna hatari kwa mwekezaji kuamua kuwekeza kwenye kampuni bila ya kufanya uchunguzi yakinifu kuhusu kampuni hiyo. Kuwekeza kwenye kampuni kwa kufuata bei ya hisa tu si sahihi, mwanahisa unashauriwa kufuata uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa kunyambulisha mahesabu ya kampuni, hii itakupa nafasi nzuri ya kujua unawekeza kwenye kampuni ya aina gani na ujtarajie mrerjesho mzuri wa mtaji uliowekeza.
Kwenye kulinganisha kwamba ni kampuni gani uwekeze ni vizuri ujue mtaji wa kampuni husika, idadi ya wanahisa, idadi ya hisa zilizotolewa au zilizoko sokoni, na gharama za uendeshaji. Hapo utaweza kujua kwa nini kampuni moja inatoa gawiomla shilingi mia mbili kwa hisa na nyingine inatoa gawio la shilingi saba kwa hisa.
Ni vizuri pia wanahisa kuodokana na dhana ya uwekezaji wa muda mfupi, hii itakupa msukumo hasi wa kuuza hisa kwa bei ha hasara ili kurtejesha mtaji. Uwekezaji wa muda mrefu yaani kuanzia miaka 5 na kuendelea ni uwekezaji mzuri kwani licha ya mtaji wako kuendelea kukua pia unaongeza thamani ya hisa zako kwa muda wote huo pamoja na kupata gawio la kila mwaka.
Kila la heri ndugu wanahisa kwa uwekezaji bora kwenye soko la hisa.
Chanzo: Mwanahisa - CRDB BANK PLC. Toleo la Novemba, 2012.
Subscribe to:
Posts (Atom)