Sunday, December 23, 2012

JE NI WAKATI GANI WA KUNUNUA HISA WENYE MANUFAA ZAIDI KWA MWEKEZAJI?

Kwa Mwanahisa kujua hasa ni wakati gani wa kununua hisa, hiyo tayari ni sehemu ya uwekezaji katika Soko la hisa la Dar es salaakm. Lakini wawekezaji wengi wa ndani hawaoni fursa hii kwa kukosa au kutokuwa na taarifa/maarifa muhimu kuhusu uwekezaji kwenye hisa. Moja ya wakati mzuri wa kuwekeza kwenye hisa ni pale ambapo kampuni inato hisa zake sokoni ili kuongheza mtaji wake (Initial Public Offers - IPO), wakati huo hisa huuzwa kwa bei ya chini na baada ya daftari la hisa kufungwa na kupelekwa kenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE) wawekezaji hao huziuza hisa hizo kwa bei ya juu na kupzta faida. Hii ni njia mojawapo ya kuopngeza faida kwa haraka, na hatari yha kupoteza thamani ya uwekezaji inakuiwa ndogo hasa pale wawekezaji (wanunuzi wa hisa) wanapokuwa wengi katika soko la hisa. Licha yahiyo kuna njia nyingine ambazo zinarudisha faida nzuri kwenye uwekezaji wa hisa. Mojawapo ni pale ambapo bei ya hisa kwenye soko inakuiwa imeshuka au iko chini, ila ni muhimu kufanya utafiti au kufuatilia mahesabu ya kampuni unayotaka kuwekeza au kwa kutumia wataalamu wa masuala ya fedha (financial analysts). Bei ya hisa kupanda au kushuka katika soko, ni jambo la kawaida na inasababishwa na mambo mengi. Mambo mawili makubwa ni kwamba, kampuni haifanyi vizuri na wawekezaji wake wameamua kuondoa mitaji yao kwenye hiyo kampuni na kuacha kuwekeza. Hii utaijua iwapo utakuwa unafuatilia kwa undani utendaji wa kampuni na siyo tu kuangalia bei ilioyoo sokoni. Jambo la pili ni kwamba, bei ya hisa inaendeshwa kutokana na nguvu ya soko inayoendeshwa na wanunuzi na wauzaji wa hisa. Hapa bei ya hisa inakuwa haiendani na utendaji wa kampuni. Utakuata kampuni inatengeneza faida kila mwaka na mahesabu yake yako wazi kuonyesha ufanisi wake , bado bei inakuwa chini. Huo ndio wakati mzuri wa kununua hisa kwa sababu pamoja na kwamba bei ya hisa za kampuni hiyo ziko chini ya bei iliyouzwa sokoni kwa mara ya kwanza, lakini bado kampuni inatengeneza faida. Hisa hizi zinakuwa ni nafuu na rahisi kulinganisha na thamani halisi ya hisa. Ni muhimu sana kwa wawekezaji katika hisa kusoma kwa undani mahesabu na mwenendo wa kampuni wanayotaka kuwekeza kabla ya kufanya maamuzi ya kununua au kuuza hisa zo. Kwa upande mwingine kuna hatari kwa mwekezaji kuamua kuwekeza kwenye kampuni bila ya kufanya uchunguzi yakinifu kuhusu kampuni hiyo. Kuwekeza kwenye kampuni kwa kufuata bei ya hisa tu si sahihi, mwanahisa unashauriwa kufuata uchunguzi uliofanywa na wataalamu wa kunyambulisha mahesabu ya kampuni, hii itakupa nafasi nzuri ya kujua unawekeza kwenye kampuni ya aina gani na ujtarajie mrerjesho mzuri wa mtaji uliowekeza. Kwenye kulinganisha kwamba ni kampuni gani uwekeze ni vizuri ujue mtaji wa kampuni husika, idadi ya wanahisa, idadi ya hisa zilizotolewa au zilizoko sokoni, na gharama za uendeshaji. Hapo utaweza kujua kwa nini kampuni moja inatoa gawiomla shilingi mia mbili kwa hisa na nyingine inatoa gawio la shilingi saba kwa hisa. Ni vizuri pia wanahisa kuodokana na dhana ya uwekezaji wa muda mfupi, hii itakupa msukumo hasi wa kuuza hisa kwa bei ha hasara ili kurtejesha mtaji. Uwekezaji wa muda mrefu yaani kuanzia miaka 5 na kuendelea ni uwekezaji mzuri kwani licha ya mtaji wako kuendelea kukua pia unaongeza thamani ya hisa zako kwa muda wote huo pamoja na kupata gawio la kila mwaka. Kila la heri ndugu wanahisa kwa uwekezaji bora kwenye soko la hisa. Chanzo: Mwanahisa - CRDB BANK PLC. Toleo la Novemba, 2012.

Monday, August 20, 2012

VIKWAZO DHIDI YA USINGIZI MURUA NA SULUHU ZAKE

Usingizi ni moja kati ya vitu muhmu kwa afya ya binadamu. Kukosa usingizi ipasavyo (masaa 6-8) hupelekea matatizo kama uchovu siku inayofuata, kusinzia siku inayofuata, kupungua uzito, kupungua kinga ya mwili n.k. Kuna imani potofu ya kwamba watoto ndio wanaopaswa tuu kulala muda fasaha.

Kwa kuwa watu wengi hawapo makini katika kuangalia mienendo ya maisha yao, hawawezi kujua sababu zinazopelekea matatizo hayo, hivyo kukosa sululuhu ya kudumu. Zifuatazo ni sababu zinazopekea ukosefu wa usingizi, baada ya kuzijua itakuwa rahisi kwa mtu kukabiliana na changamoto.

Kula chakula kingi muda mchache kabla ya kulala.

Kula chakula kingi, hususani nafaka, muda mfupi kabla ya kulala hufanya mwili utumie nishati nyingi katika kumeng'enya chakula, hivyo kuvuruga utaratibu wa nishati wa mwili. Pia kunywa maji kabla ya kulala humfanya kuamka usiku ili kujisaidia, hivyo kubadili utaratibu wa usingizi.
Mtu anapaswa kula chakula chepesi na maji kidogo angalau nusu saa kabla ya kulala.

Kulala mazingira duni.

Kulala katika mazingira yanayokinzana na utu wa mtu huvuruga utaratibu wa mwili. Mazingira kama; chumba chenye mwanga mkali, chumba chenye joto au baridi kali, kulala kwenye kelele, kulala kwenye godoro laini au gumu sana, chumba kisicho na hewa safi ya kutosha n.k humfanya mtu kukosa usingizi.

Kubadili mfumo wa maisha.

Kubadili mfumo wa maisha na ambao ulikuwa umezoelewa na mwili hutatiza usingizi. Kwa mfano; kumpoteza ndugu au rafiki wa karibu, kuanza kazi mpya, kufanya kazi ngumu, kuingia kwenye ndoa, kuwa na msongo mawazo n.k huwafanya watu wengi kukosa usingizi.
Hali hii huchukua siku chache, ikiwa kama ukosefu wa usingizi itachukua muda mrefu, mtu anapaswa kufanya tahtmini ya kina.

Mazingira duni ya kijamii.

Mazingira duni ya kijamii kama; kulala zaidi ya mtu mmoja kwenye kitanda kimoja, kulala na mtu msumbufu hususani mtoto mdogo, kulala chumba kimoja na mtu anayekoroma, kulala na mtu anayesumbua usiku, kulala chumba chenye wadudu kama chawa, kunguni, viroboto n.k.
Mazingira haya yanasababishwa na umasikini wa kipato.

Matumizi ya madawa.

Kuna aina nyingi sana ya madawa ya hosptalini ambayo, pamoja na kutibu au kupunguza maumivu, hupelekea kukosekana kwa usingizi. Madawa hayo ni kama madawa ya kupunguza maumivu, kupunguza mawazo, madawa ya usingizi n.k.
Mtu anapaswa kusoma maelekezo au kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa yoyote ile ili apate kujua madhara yake na jinsi ya kuyakabili.

Matumizi ya vinywaji baridi na sigara muda mchache kabla ya kulala.

Vinywaji baridi vina kokaini, chai au kahawa ambayo huongeza msukumo wa damu. Matumizi ya vinywaji hivyo kabla ya kulala kukatiza usingizi. Kwa upande wa sigara, ikilinganishwa na watu wasiovuta sigara, watu wanaovuta sigara hukawia kupata usingizi, hivyo, kupata masaa machache ya kulala.
Kuna watu wamezoea kunywa pombe ndipo wapate usingizi, watu hawa ni watumwa wa pombe na wengi wao hutumia pombe kali, baada ya muda, pombe haitoweza kumsabishia usingizi kabiasa au akiwa hana hela ya kununua pombe mtu huyo hatoweza kulala.

Kwa kiasi kikubwa, sababu za ukosefu wa usingizi zipo chini ya uwezo wa binadamu, hivyo, mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla inapaswa kutengeneza mazingira yanayopekekea usingizi murua, mafanikio ya mtu katika kazi za kujiletea maendeleo, hutegemea, pamoja na mambo mengine, kiasi cha mapumziko anayopata kila siku kupitia usingizi.

Monday, August 13, 2012

MUUNDO WA MPANGO WA MAENDELEO

Watu wengi hushindwa kufikia malengo waliyojiwekea kwa kuwa, moja ya sabau ni, kushindwa kupanga. Kushindwa kupanga hupelekea kushindwa kutekeleza hivyo malengo kutikiwa. Zifuatazo ni hatua muhimu za kumsadia mtu pindi apangapo mradi wa maendeleo.

1. Kununua kitabu cha mipango. Mtu anapaswa kununua kitabu kidogo kwa ajili ya kuratibu na kutunza kumbukumbu za kila siku za mtu binafsi. Vitabu hizi vipo takribani kila duka la vifaa vya shule na ofisini, hujulikana kama "diary" kwa lugha ya Kiingereza.

2. Kuandika mtizamo, lengo au matarajio ya mradi husika. Mtu anapaswa kuandika mradi wake kwenye ukurasa wa kwanza wa kitabu cha mipango. Lengo husika linapaswa kuandikwa kwa herufi kubwa na kwa lugha fasaha. Kwa mfano, LAZIMA NIANZISHE MRADI WA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI IFIKAPO MWEZI JANUARI MWAKANI . Mtu anapaswa kuhakikisha anaandika lengo moja tu! Ili iwe rahisi kutekeleza.

3. Kuandika kwa kifupi shughuli muhimu zitakazofanyika na muda mahususi wa kuzifanya ili kufikia lengo kuu. Shughuli hizo hujumuisha malengo madogo madogo. Kwa mfano:

Ni lazima nianzishe mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji kabla ya mwezi Januari mwakani. Ili kufanya hivyo ninapaswa kufanya yafuatayo; (i) kuomba ushauri kutoka kwa mfugaji maarufu wa kuku wa kienyeji juu ya gharama muhimu wiki ya tatu ya mwezi Agosti (ii) kukamilisha gharama muhimu za kuanza mradi kabla ya wiki ya nne ya mwezi Agosti, kama ikibidi (iii) kuomba ushauri kutoka kwa Afisa Mifugo juu ya aina bora ya kuku, magonjwa n.k wiki ya kwanza ya mwezi Septemba (iv) kufanya utafiti juu ya upatikanaji wa soko la kkienyeji ndani ya wiki ya pili na tatu ya mwezi Septemba (v) kuanza kujenga banda wiki ya tatu ya mwezi Septemba na kukamilisha kabla ya mwisho wa mwezi Oktoba (vi) kununua chakula na dawa muhimu wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi Novemba (vii) kununua kuku wa kienyeji; mitetea nane na jogoo mmoja wiki ya kwanza ya mwezi Desemba. Hivyo kuanza ufugaji rasmi kabla ya mwezi Januari.

Mpangilo wa shughuli na muda hutegemea mazigira, uelewa wa mtu, rasilimali akizo nazo n.k. Kwa mfano, kupata mtaji kwa mtu mmoja ikawa changamoto ili hali, kwa mtu mwinine kupata ushauri ikawa changamoto kuu.Mtu apange shughuli rahisi kisha shughuli ngumu baadaye kadiri ya uwezo wake. Ni bora kumshirikisha mtu wa karibu ambaye nimzoefu wakati wa kupanga ili kuepuka kupanga shughuli isiyotekelezeka ndani ya muda fulani.

4. Kurudia kusoma, kufanya marekebosho na kukariri mwongozo ulioandaliwa. Muongozo uwekwe maeneo ambayo ni rahisi kuuona na kuusoma kama kwenye pochi au kwenye mkoba. Hii itaongeza hamasa ya kusoma na kutaka utekelezaji.

5. Kuanza utkelezaji kwa kuandaa ratiba ya hughuli iliyopangwa kufanyika ndani ya muda husika. Katika hatua hii mtu anapaswa kuwa makini sana ili asiruke shughuli aliyoipanga. Ikiwa kama shughuli husika haikuisha ndani ya muda uliopangwa, basi ipelekwe mbele. Kuruka hatua kutasababisha kuvuruga mpango mzima.

6. Kufanya uchambuzi wa hatua kwa hatua. Mtu anapaswa kuangalia utekelezwaji hatua iliyopita ili kufanya marekebisho kwa hatua zitakazofuata kabla mambo hayajawa magumu. Mwenye mradi anapaswa kuwaongoza kwa makini wasaidizi wake wa kila siku.

Monday, August 6, 2012

VIASHIRIA VYA BAHATI

Watu wengi hufikiri ya kwamba bahati (nzuri au mbaya) hujijia tu, haibashiriki na ni vigumu kuzuia. Hiyo ni kwa kuwa hawajui maana halisi ya bahati. Ikiwa kama mtu hajui maana halisi ya bahati ni vigumu kuitawala. Waswahili wanasema "mtembea bure si sawa na mkaa bure" pia "bahati ya mbwa ipo kwenye miguu yake".

Bahati ni kujitambua dhidi ya uhalisia. Bahati ni kuwa na hisia chanya juu ya tukio au jambo fulani. Mtu mwenye hisia chanya huona kila kitu kinamtumikia (kila kitu kinamsadia kufanikiwa), kwa upande mwingine, mtu mwenye hisia hasi huona kila kitu kinampiga vita; kila kitu huonekana ni kikwazo.

Kiasi cha imani (nguvu itokayo ndani) huamua kiwango cha hisia na bahati ya mtu. Mtu anapofanya jambo lolote pasipo imani, kufanya jambo kwa mashaka makubwa, huwa na uwezekano mkubwa kufanya makosa ya kizembe hivyo kujiweka katika nafasi kubwa ya kungeza vikwazo au kukosa kabisa kile alichotaka. Pindi mtu anapojiamini kwa kiasi kikubwa ndipo uwezekano wa bahati (kufanikiwa) unapoongezeka.

Kwa kiasi fulani, bahati hutegemea maarifa. Mtu mwenye maarifa hufanya kazi kwa uhuru. Ni vigumu kutenganisha bahati na maarifa; kwani ili kufanya kitu kwa usahihi uwezo wa mtu husika kufuata sheria na kanuni ipasavyo unahitajika.

Kwa kuwa bahati hutegemea imani, mtu anapaswa kuwa makini na kiwango cha imani yake wakati anapofanya jambo lolote lile. Ikiwa kama kiwango cha imani ni kidogo, yafaa kusitisha kufanya jambo hilo, au kufanya hatua kwa hatua na kwa umakini mkubwa kama haiwezekani kusitisha shughuli husika.

Watu wanaolazimisha kufanya jambo bila ya imani nalo hujikuta wakifanya makosa bila ya kujitambua, kusahau hatua za kufuata, kushindwa kujitetea pindi wanapotakiwa kijitetea, hivyo kubaki wakijilaumu kwa kujisemea "nina bahati mbaya".

Kukosa umakini kimawazo huwafanya watu kudharau mambo ya msingi; kujikuta wakifanya mambo wasiyotayatarajia kisha kutokufanikiwa. Ili kuongeza nafasi ya bahati ya kufanikiwa yapaswa kuwekeza kimawazo, kushirikisha maarifa kwenye kazi ifanyikayo kwa wakati husika. Kuwekeza kimawazo husaidia kutumia rasilimali kwa ufanisi zaidi.

Takribani watu wote (wanasayansi mashuhuri, wafanyabiashara wakubwa, wasomi n.k) waliofanikiwa, walifanikiwa kwa kuwa kiwango chao cha imani kilikuwa juu. Kufanya kazi bila ya i tiketi ya kushindwa. Mtu anayetaka bahati nzuri huchagua mtizamo chanya, mtizamo chanya huongeza nishati na kusadia jitihada za kufanikiwa.

Kila mtu anayo nafasi ya kufanikiwa, watu wengi hawajui maana na jinsi ya kulinda nafasi wanazopata katika maisha. Bahati nzuri ipo, na kila mtu anao uwezo wa kuitawala. Kwa kulitambua hilo, hakuna haja ya kuogopa kufanya jambo lolote kwa kuwa hakuna bahati mbaya.

Monday, July 30, 2012

MIKAKATI YA KUONDOKANA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Idadi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja inaongezeka kwa kasi. Nchi kadhaa, hususani za Ulaya na Marekani zimehalalisha 'ndoa' za aina hiyo kwa kigezo cha haki za binadamu, huku zikizishinikiza nchi changa kufanya hivyo.
Wanaume wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wenzao wanaitwa mashoga, huku wanawake wakiitwawasagaji. Kuna baadhi ya mashoga na wasagaji wasiopenda hali yao ya kimapenzi ila hawajui wataachaje. Zifuatazo ni baadhi ya mbinu za kuondokana na uovu huu.

1. Kutafakari mpango wa Mungu.

Kila shoga au msagaji anapaswa kutafakari azma ya Muumba wake; azma ya Mungu itafakariwe sambamba na matendo anayotenda. Mungu alimuumba mtu mme na mtu mmke ili wazaliane, kumheshimu na kumtukuza. Mungu hakumuumba mtu ili amwoe mtu wa jinsia yake, na kufanya hivyo ni kukiuka maagizo ya Mungu, na hakuna msamaha kwa mtu anayevunja amri ya Mungu. Kwenda kinyume na mpango wa Mungu ni usaliti, adhabu ya usaliti ni kubwa sana.

2. Kuomba msaada kutoka kwa wataalamu.

Kuondokana na hali ya ushoga au usagaji kunawezekana ikiwa kama kila mshiriki ataomba ushauri na tiba, hususani tiba ya akili, kutoka kwa wataalamu wa saikolojia. Pia viongozi wa dini wanao mchango mkubwa sana, kwani, kwani wanauwezo wa kutoa mafunzo ya hatua kwa hatua, kulingana na imani ya mwathirika hata atapopona. Mtu husika anapaswa kuvunja ukimya.

3. Kuweka dhamira ya kuacha.

Hakuna lisilowezekana chini ya jua. Ikiwa kama mshiriki wa mahusiano ya jinsia moja atadhamiria kwa dhati kuacha, atafanikiwa. Kufanikiwa au kutafanikiwa kunategemeana na maamuzi ya mtu. Shoga au msagaji anapaswa kufanya magumu kwa kutumia msaada kutoka kwa watu wa karibu; watu wanaotoa msaada wa hali na mali na kwa mapenzi mema.

4. Kukwepa mazingira hatarishi.

Shoga au msagaji anapaswa kukwepa mazingirompa vishawishi, ikiwamo kuwakwepa mashoga au wasagaji, kukwepa m,aeneo aliyokuwa akikutana na wenzake, na kupenda kukaaa maeno yanayotumiwa watu wa jinsia zote. Marafiki na mazingira huwafanya watu kuingia maovuni, vivyo hivyo, huwafanya watu kukwepa uovu.

5. Kujiamini

Shoga au msagaji napaswa kujenga utashi kutoka ndani. Utashi imara unategemea mawazo chanya juu ya jambo husika. Manneno yanohusiana na udhaifu na kukata tamaa hayatakiwi kabisa; maneno kama "siwezi kuacha...", hatatakiwi kabisa. Maneno ya ujasiri na kujikupewa kipaumbele muda wote, maneno kama "mimi ni mwanamke, mimi ni fahari ya ulimwengu nitadhihirisha hivyo kwa kuacha usagaji", "wanaume hawashindwi na kitu, mimi ni mwanaume, mini sitoshindwa kuacha ushoga".

6. Kuangalia vivutio vya jinsia tofauti

Msagaji anapaswa vivutio bna thopata mwananmke asiye msagaji kutoka kwa jamii, pia vivutio kutoka kwa mwanaume kama sauti, misuli n.k pia shoga anapaswa kungaliasio mashoga, vivutio kutoka kwa mwanamke kama sura, mwendo n.k. Jinsia zote mbili zri thamani ya kulea familia katika maadili mema, kuwa na watoto na kuitwa baba au mama.

7. Kutolaumu matukio ya siku za nyuma.

Matukio kama unyanyasaji wa kijinsia aliowahi kufanyiwa mtu siku za nyuma, hususani wakati wa utoto, huleta changamoto katika kuacha kile mtu anachoamini mtu kinampa furaha. Ikiwa kama shoga aliwahi kunyanyaswa kijinsia, anapaswa kuamini ya kwamba aliyefanya hivyo alitumwa na shetani, na ni sehemu ya mapito ya mwanadamu.

8. Kusoma kutoka kwa walioshinda

Kuna simulizi na machapisho mengi kutoka kwau waliofanikiwa kuepa uovu huu. Mshiriki anapaswa kusoma ili kuipata mbinu bora zaidi, ikiwa ni pamoja na kuombna ushauri pale anapokumbana na changamoto kubwa; changamoto inayotishia kuzima juhudi zake za kuacha. Kupitia Google kuna toviuti za mashirika au vikundi vingi vinavyojihusisha na kuwasaidia watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ili waweze kuacha.
KILA KITU KINAWEZEKANA, KUACHA MAPENZI YA JINSIA MOJA INAWEZEKANA!

Monday, July 23, 2012

MISINGI YA KUWALINDA WATOTO DHIDI YA MAPENZI YA JINSIA MOJA

Janga la mahusiano ya kimapenzi baina ya watu wa jinsia moja ni changamoto kubwa sana katika malezi ya watoto. Kwa kiasi kikubwa mapenzi ya jinsia moja huchangiwa na sababu za kimazingira na chaguo la mtu husika. Japokuwa, kwa kiasi kidogo, aina hii potofu ya mahusiano inachangiwa na sababu za kibailojia.
Hali ilikuwapo kabla hata ya kuzaliwa Yesu Kristo. Yote kwa ypote, ni lazima kupambana na hali hii na kuishinda. Misingi ifuatayo yafaa kutumiwa na wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ili kuwalinda watoto dhidi ya janga la mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja.

1. Kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.

Wazazi na walezi wanapaswa, kwa nguvu zao zote, kuhakikisha usalama wa watoto. Kuwalinda watoto wasitendewe unyama dhidi ya jinsia yao kama kama ulawiti na ubakaji.

Kwa mfano, mtoto wa kike aliyebakwa hujenga chuki dhidi ya wanaume, hivyo hukua na hasira dhidi ya mwanaume yeyote yule hata atakapokuwa mkubwa. Kutokana na chuki dhidi ya wanaume, mtoto huyo huimarisha mahusiano hususani ya kimapenzi dhidi ya wasichana mwingine mwenye chuki dhidi ya wanaume kama alivyo yeye. Lengo la kufanya hivyo ni kutaka kutimiza mahitaji yao ya kimapenzi.

Unyanyasaji mkubwa wa kijinsia hufanyika majumbani; unyanyasaji wa kijinsia hufanywa na watu wanaoheshimika kama baba wa kambo, baba mdogo, mjomba, shangazi, mfadhili n.k. Hivyo, wazazi na walezi wanapaswa kuwa makini sana dhidi ya watu wanaoishi au kuwalea watoto wao.

2. Kuwakuza watoto katika jinsia zote.

Wazazi ndio shule ya kwanza kwa watoto. Watoto hujifunza kutoka kwa wazazi maana na majukumu ya baba na mama (au mme na mke).
Hivyo, baba anapaswa kuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa watoto wa kiume, na mama kuwa mfano mzuri wa kigwa kwa mtoto wa kike kupitia maisha yao ya kila siku.

Ikiwa kama ni vigumu kwa mzazi mmoja kushiriki katika malezi, mtoto wa jinsia husika atengewa mazingira yatakayomwezesha kuiga na kuishi kadiri ya jinsia yake. Kwa mfano, kupata nafasi ya kuona jinsi familia za jirani zinavyoishi.

3. Kutomkaripia mtoto vikali kutokana na tabia yake.

Wazazi na walezi wananapaswa kuwa makini pale wanapowaonya watoto wao kwa kuwa wameonyesha tabia au mienendo hatarishi. Kwa mfano, kutompiga vikali mvulana kwa kuwa anajiremba au kuiga sauti za wasichana.
Makaripio makali huwafanya watoto kukubuhu na kujenga kiburi, na hivyo kuamua kuendeleza tabia husika.

Wazazi na walezi wanapaswa kujua ya kwamba watoto, hususani wakati wa balehe au kuvumja ungo, ni watundu sana na hupenda kuiga kila kitu. Hivyo, wazazi na walezi wanapaswa kuwa na upole huku wakiwafundisha madhara ya tabia hatarishi.

4. Kutoa fursa sawa kwa jinsia zote za watoto.

Watoto huwa njiapanda nyingi hususani wakati wa balehe au kuvunja ungo. Baadhi ya watoto huona ya kwamba jinsia tofauti na yao inapata faida sana. Hivyo huanza kuiga mitindo yao ya maisha, mingi ya mitindo hiyo ikiwa ni hatarishi.

Kwa mfano, watoto wa kike huona watoto wa wakipewa uhuru wa kwenda watakapo, kutopangiwa majukumu au kazi nyingi za kifamilia n.k. Hivyo, wasichana hao huiga mienendo ya kiume ili kujiridhisha. Tabia hii ikiachwa huwafanya wasichana hao kujihususisha kimapenzi na wasichana wenzao. Wazazi na walezi wanapaswa kutoa fursa sawa kwa wote ili watoto wote wafurahie jinsia zao tangu awali.

5. Kuwalea watoto kwa misingi ya dini.

Wazazi na walezi wanapaswa kuwalea watoto kwa misingi ya imani zao. Ili kufanikisha hilo, wazazi na walezi wanapaswa kuishi kandiri ya imani zao ya kila siku.
Malezi ya kidini huwafanya watoto kuona muhimu wao kwa mujibu wa jinsia zao.

Kwa mfano, wazazi kuwasimulia watoto habari za watu maarufu waliomtumikia Mungu katika dini husika kwa jinsia. Pia kuwaambia watoto ya kwamba Mungu alimuumba mtu mke na mtu mme ili wamtumikie.

6. Kuwalea watoto kwa mujibu wa jinsia zao.

Mtoto wa kiume anapaswa kulelewa kama mtoto wa kiume ili aweze kuwa mwanaume, na mtoto wa kike vivyo hivyo. Hata kama mtowazazi waliyoipendelea, mtoto aliyezali maadili mema na mwenendo unaokubalika.

Kwa mfano, ikiwa wazazi walipendelea mtoto wa kwanza awe wa kike, na akazaliwa mtoto wa kiume; wanapaswa kumlelea mtoto huyo kama wa kiume, na si kumdekeza. Watoto wengi wa kiume wanaodekezwa huwa mashoga.

Ikiwa kama wazazi na walezi (jamii kwa ujumla) watafanikiwa kuwalea watoto kwa misingi hiyo; kabla ya mtoto kuanza maisha tofauti na ya familia, kwa mfano kwenda shule ya kulala (bodi), changamoto ya mapenzi ya jinsia moja itakuwa imepunguzwa au kumalizika kabisa. Takwimu zinaonyesha kwamba watu wenye mahusiano ya jinsia huimarika wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Monday, July 16, 2012

MBINU ZA KUUKABILI USHIRIKINA

Ushirikina ni hali ya kuamini kuna haja ya kuwa na nguvu ya ziada kutoka kwa mtu au nafsi ili kuweza kufanikisha jambo fulani. Kwa mfano, kuamini kuna haja ya kufanya kafara (kuchinja na kumwaga damu ya mtu au mfugo) ili kuweza kupata kazi. Imani za ushirikina ni maarufu katika jamii na sehemu mbalimbali duniani.

Imani za ushirikina ni kukwazo kikubwa kwa jamii nyingi kwa kuwa:

Hupunguza nafasi za kusoma. Kuamini katika ushirikina kutochukua jitihada za kusoma ili kupata suluhu juu ya changamoto zinazoikabili jamii husika. Kwa mfano, kutegemea ushirikara kunaweza kuwazuia wafanyabiashara kutofanya tafiti mpya juu ya mwenendo wa biashara, hatimaye hufilisika.

Huongeza mzigo. Kuamini ushirikina kunamfanya mtu kuishi akiwa amevaa vitu mbalimbali ili kutimiza malengo, mfano, kuvaa irizi. Vitu hivyo kwa ujumla wake huongeza mzigo katika mwili wa mtu.

Huzuia malengo kutimia. Watu wanaoamini ushirikina huacha kufanya mambo waliyoyapanga kwa kuwa masharti hayaruhusu. Kwa mfano, mtu anayekwenda kufanya biashara fulani, akikutana na bundi asubuhi, kwa kuwa anaamini bundi ni ishara ya mkosi, mtu huyo hurudi nyumbani, hivyo, kuacha kufanya biashara kwa siku husika.

Huleta mfadhaiko. Ikiwa kama mtu anaamini irizi ndio kinga yake, kwa bahati mbaya akasahau kuvaa irizi siku fulani, siku hiyo ataishi kwa wasiwasi na hofu siku nzima. Au mtu akiamini mzee fulani ni mchawi, na akakutana nae, mtu huyo hupata mfadhaiko kwa kuogopa atakuwa amelogwa.

Huongeza changamoto za kimaisha. Kutokana na kuamini ushirikina, mshirikina hujinyima fursa nyingi za kusonga mbele. Kwa mfano, mtu anayeamini ya kwamba jirani yake ni mchawi, mtu huyo hukatisha mawasiliano na jiarani yake, pia, mtu huyo anaweza kuwaacha watoto wake bila ya uangalizi wowote kwa kuogopa wanawe watalogwa na jirani yake.

Mbinu za Kukabili Imani na Madhara ya Ishirikina.

Inawezekana kabisa kuepa ushirikina, na mtu husika asidhurike kwa kufanya yafuatayo:
Kutumia takwimu.
Ili kukwepa mawazo au uhusishwaji wa tukio fulani na imani za kishirikina, mtu anapaswa kusoma takwimu dalili n.kuhusu tukio husika. Kwa mfano, ili kutohusisha kifo na ushirikina, mtu anapaswakusoma takwimu kuhusiana na kifo cha mtu husika.

Kutafuta ushauri.
Ili kupunguza uwezekano wa madhara fulani kutokea mtu anapaswa kuomba na kufuata ushauri kutoka kwa wataalamu. Kwa mfano, ili kukwepa hasara katika biashara, mfanyabiashara anapaswa kutafuta na kutekeleza ushauri kutoka kwa wataalamu wa biashara kabla na wakati wa biashara husika.

Kujaribu nguvu ya ushirikina.
Ikiwa kama mtu anaamini ya kwamba bila ya kuwa na irizi hawezi kufanya vizuri katika mchezo, mtu huyo afanye maandalizi sahihi huku akiwa na imani ya kuwa atafanikiwa bila ya kukumia kizizi. Pia mtu huyo anaangalie kama mara zote anazotumia irizi je anakiwa? Kama kizizi ndio suluhu ya kufanikiwa, je kuna haja gani ya kufanya mazoezi?

Kumwamini Mwenyezi Mungu.
Kila kitu (kinachoonekana au kisichoonekana) kimeumbwa na Mungu. Mungu ndiye mtawala wa kila kitu. Ikiwa kama Mwenyezi Mungu ameweza kuumba kila kitu, je atashindwaje kushinda hila za ushirikina?

Ikiwa kama mambo hayaendi kama mtu alivyopanga, haimaanishi ya kwamba Mungu ameshindwa, bali kwa namna moja au nyingine Mungu anatoa somo. Kwani kutokana na matatizo yanayomkabili mtu, ndipo watu huamini na kutii uwepo wa Mungu. Kupiga magoti kwa Mungu na kufanya kazi kwa bidii ndiko kunakoleta suluhu ya kudumu.

Achilia mbali mila na tamaduni, imani za ushirikina zinachukua nafasi kubwa katika jamii kwa kuwa watu hawana suluhu dhidi ya changamoto zinazowakabili. Kwa mfano, kukosekana kwa elimu na tiba juu ya ugonjwa fulani unaosababisha vifo vingi, huwafanya watu katika jamii husika kuhusisha ugonjwa huo moja kwa na imani za ushirikina.

Monday, July 9, 2012

MBINU ZA KUPUNGUZA MAKALI YA MAJANGA

Hakuna mtu yeyote mwenye kinga dhidi ya janga lolote lile! Majanga huwakabili watu bila ya kubagua na mtu anapaswa kuyakabili bila ya kusita. Takribani mara zote majanga husababishwa na mahusiano ya kimapenzi, kazi, mabadiliko ya kiuchumi, ajali, mabadiliko ya afya n.k

Kiasi cha ukubwa wa janga au madhara yatokanayo hutofautiana sana; kikubwa ni kwamba kuna tofauti kubwa sana juu ya hisia na mbinu za kukabili janga husika. Kuna watu huwa na hisia chanya katika kuyakabili majanga (wanaamini watashinda), huku wengine husita, hukumbwa na hofu hatimaye hushindwa.

Ili kuweza kukabili janga na kuweza kupunguza ukubwa wa madhara, zifuatazo ni baadhi ya mbinu za kufahamu na kumudu:

a) Kuamini janga halikwepeki.

Kila mtu anapaswa kujua na kukiri ya kwamba kukumbana na changamoto tete katika maisha ni sehemu ya mapito ya kiumbe hai yeyote yule, hususani binadamu. Ikiwa kama mtu amekumbwa na hali ngumu anapaswa kujua kuna wengine wenye hali ngumu zaidi.

Kwa mfano, kama mtu amesalitiwa au kuibiwa mali zake anapaswa kujua ya kwamba kuna watu walio chini ya uangalizi wa daktari (ICU) ili kunusuru maisha yao au kuna familia zisizo na makazi wala chakula kutokana na mafuriko au maporomoko ya ardhi.

b) Kutolazimisha suluhu ya haraka.

Janga fulani linapotokea watu hufanya jitihada ili kuweka hali sawa ndani ya muda mfupi au haraka iwezekanavyo. Haishauriwi kusisitiza suluhu ya haraka, kwani takribani suluhu nyingi za haraka, zinazodhaniwa kuwa ni za kudumu hutuliza maumivu tu na hivyo kuongeza ukubwa wa tatizo nyakati za usoni. Suluhu nyingi za haraka hazina umakini.

Kwa mfano, kama mtu amesalitiwa kimapenzi, na akaamua kuanzisha mahusiano mapya ndani ya muda mfupi, mahusiano hayo mapya huleta madhara makubwa au kiafya au kiuchumi isivyotarajiwa.

c) Kutolaumu historia.

Muda mfupi baada ya adha fulani kutokea, watu wengi hujilaumu wenyewe au watu wengine kwa uzembe uliofanyika. Watu wengi husema "ningejua...ninge... Kauli kama hizo hazisaidii kitu chochote katika kuleta suluhu.

Hali kama hiyo huzuiowa kwa kubadili mawazo; kwa kuamini ukweli kwamba hakuna binadamu aliyekamilika, pia watu werevu hujifunza kutoakana na makosa wa wenzao, ikiwa makosa hatafanyika, kujifunza kutafanyikaje? Majanga hutumika kama kutoa somo kwa siku zijazo.

d) Kuangalia manufaa ya tukio.

Japokuwa majanga yote ni machungu,pia katika uchungu huo kuna chembechembe ndogo sana za utamu. Chembe hizo ndogo hugundulika baada ya kuchambua mkasa kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Baada ya uchambuzi wa kina, mhanga anaweza kujua uimara na udhaifu wake. Majanga huwa ni kipimo kuzuri dhidi ya mahusiano ya mhanga na jamaa zake wa karibu.

Kwa mfano, baada ya kufilisika kiuchumi, mhanga anaweza kujua nani ni rafiki, ndugu au jamaa wa kweli; kwani undugu ni kufaana na siyo kufanana. Majanga hutoa somo kwa watu wengine juu ya mienendo ya watu wao wa karibu.

e) Kuamini suluhu itapatikana.

Kama inavyosemwa, hakuna kinachodumu milele, kila kitu kitapita, hivyo basi, mhanga anapaswa kuamini ya kwamba hata machungu aliyonayo yatapita.
Uzoefu unaonyesha ya kwamba, majanga hutisha sana siku za mwanzo, baada ya muda fulani mhanga hupata ahueni na hatimaye, kutokana na juhudi, suluhu ya kudumu hupatikana. Kwa mfano, wakati wa ajali kabla ya huduma ya kwanza hali ni mbaya ikilinganishwa na wakati baada huduma ya daktari.

f) Kuepuka mjumuisho.

Janga huathiri sehemu fulani tu ya maisha ya mtu. Kupata msukosuko katika sehemu A ya maisha haimaanishi ya kwamba sehemu B nayo itapata msukosuko na kushindwa kufanya kazi.

Kwa mfano, mtu anapoenguliwa kazini huku familia yake na ndugu zake wakimtegemea, haimaanishi kwamba mrafiki na jamaa wengine watamsaliti; kwani watu hao hutoa ushirikiano (hutoa misaada au kutafuta kazi) ili kuhakikisha maisha yanasonga mbele. Hivyo haipaswi kuona ya kwamba janga fulani litafunga milango mingine.

Monday, July 2, 2012

MBINU ZA KUEPUKA TAMAA MBAYA

Tamaa mbaya ni hali ya kutaka kumiliki mali zaidi ya mahitaji halisi; hali ya mtu kutotaka kuridhika, kwa mfano, kurudia rudia chakula ili hali watu wengine wanakosa. Tasnia ya matangazo hutumia mwanya huu kwa kutoa matangazo bora yanayoteka akili za watu na kuwaamuru watu wagombanie bidhaa ili wapate furaha, kwa lengo la kuvutia wateja.

Yafuatayo ni madhara ya tamaa mbaya:

¤ Kukosa kujitawala. Watu wenye tamaa mbaya hawawezi kumiliki hisia zao, hawawezi kutawala malengo yao; huyumbishwa na pepo za ushindani.
¤ Kushindwa kuweka malengo. Watu wenye tamaa mbaya hawawezi kuweka kipimo halisi cha malengo yao, wengi huvutwa na malengo au mipango ya wenzao ili wapate kuwashinda.
¤ Kuingia kwenye madeni. Kutaka kujilimbikizia mali kunawafanya watu kukopa kwa pupa na kulipia mambo yasiyo na tija ya kweli kwao. Madeni hayo hupelekea mtu kudhalilika na kufilisiwa baada ya kushindwa kulipa.

¤ Kukiuka maadili. Tamaa zilizopitiliza huongeza uwezekano wa mtu kukiuka miiko ya kazi au maadili ya jamii yake kama vile; udanganyifu, wizi, utapeli n.k
¤ Kuvunja mahusiano ya mtu. Tamaa mbaya huleta mtafaruku hususani pale mtu anapoingilia na kuhatarisha maslahi ya mwenzie au jamii yake. Kwa mfano kusogeza mpaka wa shamba au kiwanja.
¤ Kuleta tabia hatarishi. Tamaa mbaya hupelekea tabia hatarishi kama kukosa usingizi, kukosa hamu ya kula, hasira n.k. Hali hizo hupelekea kupungua kwa kinga ya mwili na uzito na hatimaye magonjwa.

Jinsi ya Kukwepa Tamaa Mbaya

1. kukubali mafanikio. Mtu anapaswa kutizama ubora wa mali alizo nazo, ikilinganishwa na awali, bila ya kuangalia nani anamiliki nini. Kuridhia mafanikio ni silaha muhimu sana.

2. Kujitathimini na kuweka malengo. Mtu anapaswa kujiweka mbali na hisia mbaya; hisia za kukosa, na kujiangalia kwa kina mahitaji halisi. Mahitaji halisi huwekwa kulingana na uwezo wa mtu husika.

3. Kukwepa kujithaminisha na mtu.
Mtu asifadhaike kutokana na hatua za mafanikio jamaa zake walizopiga, kwani kila mtu anapata fursa tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti. Pia kamwe mafanikio hayawezi kufanana, kwani mafanikioa ni kama vidole.

4. Kuwasaidia wengine. Kuwawazia na kuwasaidia watu wanaokosa mahitaji ya msingi kama chakula, makazi na mavazi husaidia kupunguza tamaa mbaya kwa kiasi kikubwa, hii ni ngumu sana kwa watu wenye wivu. Ni muhimu kuwasaidia yatima, wajane, wazee wasio na walezi, vilema n.k.
Katika shida na tamaabu zao.

5. Kumwomba Mungu.
Mtu anapaswa kumomba Mungu kadiri ya imani yake, kwani kila mtu anaamini Mungu yupo. Mtu anapaswa kumwomba Mungu ampatie afya, amani, utulivu wa akili na nafsi na mkate wa kila siku; kwani vitu hiyo ni bora kuliko kumiliki mali zenye thamani kubwa kama tani kadhaa za dhahabu.

Tuesday, June 26, 2012

KUJIPANGA UPYA

Watu wasiokata tamaa; watu wanaoamini kuteleza sio kuanguka; watu wanaoamini kushindwa kufikia malengo kunatoa nafasi ya kujifikiria upya juu ya mwenendo wao, marafiki, mazingira n.k ndio wanaofanikiwa.

Katika mataifa makubwa kama Marekani, mataifa yenye fursa nyingi za kufanikiwa; mataifa ambayo yamelegeza sera zao ili kumruhusu mtu afanye anachotaka, takribani 95% ya watu huwa wamefilisika kimaisha wakifika mika 65.

Inashangaza! Kuna watu huishi maisha yao ya ujana katika dimbwi la umasikini, wanakuja kupata mafanikio wakifika uzeeni, kwa upande mwingine, kuna watu wanaofurahia maisha yao ya ujana, ili hali wakifika uzeeni huishi maisha duni kabisa.

Kushindwa kufikia malengo ndani ya muda fulani haimaanishi mtu husika ana bahati mbaya, si nadhifu, hajasoma n.k, bali ni kwa sababu kuna mahali fulani na kwa namna fulani nuru yake imezimika.

Kuzimika kwa nuru kunampa mtu udhaifu. Udhaifu huo unatumiwa na matapeli, waganga wa jadi, watu wanaojiita 'manabii' n.k kumtapeli mtu kwanza kifikra na baadaye kipato kidogo alicho nacho.

Nuru (dhamira) ya mafanikio imetunzwa kwa makini katika ubongo, imetunzwa sehemu salama, kwa bahati mbaya mtu husika kwa kushirikiana na wawezeshaji wengine huizima bila ya yeye kujua.

Ikiwa kama nuru imejeruhiwa, inapaswa kutibiwa haraka sana, kabla ya ugonjwa wa kutothubutu kusonga mbele kumkumba mtu na kumsababishia 'kifo'.

Kuna misemo ya Waswahili kama: mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe, (japo kwa sasa, mtaji wa masikini ni akili yake mwenyewe), ndondondo si chururu, kimfaacho mtu chake, heri shika kenda kuliko kumi nenda rudi, n.k

Misemo yote kama hiyo inalenga kutoa ujumbe kwamba, nguvu na jitihada za mtu binafsi ndizo zinazomfanya asonge mbele, hasa katika ulimwengu huu wa ushindani. Jitihada za mtu ndio nishati ya kweli inayoweza kumvusha mtu katika kipindi kigumu katika maisha. Haijalishi mtu ana elimu kiasi gani, kama asipodhamiria kufanya kazi, yote ni bure kabisa!

Hivyo basi, baada ya mtu kuyumbishwa anapaswa kujitafakari. Kujitafakari ni rahisi ikiwa mtu ataamua kutulia mahali tulivu, huku akitafakari kwa kujiuliza maswali "nilifanya nini? Kwa nini nilifanya hivyo? Kuna nafasi zipi sikizitumia? JE NITAFANYAJE ILI NISONGE MBELE?" n.k

Baada ya tafakari, mtu husika atakuwa amepata msingi imara wa kuonga mbele huku akikwepa makosa aliyoyafanya au watu waliyoyafanya wenzake na ambayo yalichangia kumwangusha.
Mtu asiangalie alipoangukia, bali aangalie alipojikwalia.

Mafanikio ni lazima, mafanikio hawezi kujipanga baada ya au kuona dalili za kukwama au kukwama.
MAFANIKIO NI LAZIMA! BINADAMU HAKUUMBA KUSHINDWA. NI LAZIMA MIMI KUFANIKIWA

Monday, June 18, 2012

MBINU ZA KUWINDA AJIRA (3)

5. KUPATA AJIRA YA KUDUMU.
Ni vigumu kupata au kuwa na uhakika wa kupata ajira ya kudumu, hususani katika taasisi binafsi. Hata hivyo, kuna watu wachache waliomudu kuwa na uhakika wa kufanya kazi katika kampuni au taasisi husika kwa muda mrefu; hata kuwa mtu muhimu sana katika eneo la kazi.

Ili kuwa na uhakika wa kufanya kazi kwa muda mrefu, mtu husika anapaswa:

(a) Kujiendeleza katika fani husika.

Kujiendeleza kitaaluma ni muhimu sana. Kujiendeleza kunaweza kwa kuhudhuria semina, kusoma vitabu, kuhudhuria makongamano.
Watanzania wengi hawapo tayari kulipia gharama zao binafsi ili kujiendeleza; hawapo tayari kununua na kusoma vitabu, kulipia na kuhudhuria makongamano au semina n.k. Hivyo hujikuta wakidumaza fani zao na utendaji kazi wao.

(b) Kujitolea

Kuna wakati mgumu katika maisha; wakati ambao mtu analazimika kutafuta kazi huku hajui aazie wapi.
Katika kipindi kama hicho mtu anapaswa kutafuta mahali atakapofanya kazi kwa muda kama mfanyakazi wa kuijtolea huku akipewa malipo kidogo kama nauli.
Kujitolea kufanya kazi kutamfanya mtu apate 'mitandao' ya ajira, kumwondolea msongo mawazo, kuongeza maarifa n.k. Kufanya hivyo kutamsaidia mtu kupata ajira ya kudumu kwa haraka.

(c) Kuunda mitandao

Watu wengi hupata kazi kutoka kwa watu wanaofahamiana nao. Kupata ajira kunahitaji kufahamika zaidi ya kuwa na uweledi katika fani husika.
Mtu anapaswa kuwa na kundi la marafiki katika nyanja tofauti tofauti za maisha, na marafiki wenye madaraka na ushawishi tofauti ambao watamuuunganisha na nafasi za ajira wakati wiowote anapotaka ajira.
Kutoka hatua moja kwenda nyingine kuna mlango. Mlango huo ni mtu na hufunguliwa na mtu.

(d) Kukwepa mawazo hasi.

Mawazo hujenga! "Awazalo mjinga, ndilo litakalomtokea". Ikiwa kama mtu atapokea na kuhifadhi mawazo hasi, ajue anajidumaza. Mawazo chanya huongeza rutuba katika ukuaji wa mtu.
Kwa bahati mbaya, binadamu tumezungukwa na mawazo hasi takribani kila tuishipo. Adui mbaya ni yule anayedhamiria kwa makusudi kumvunja mtu nguvu/ hamasa mtu mwingine.
Undugu huja bila uchaguzi, ila marafii huchagulika. Ikiwa mtu ameambiwa na mtu mmoja 'HUTOFANIKIWA' anahitaji watu kumi na sita kumwambia 'UTAFANIKIWA' ili kumrudishia hari.

(e) Kuheshimu kanuni na masharti.

Kwa watu wenye kazi wanapaswa kufanya kazi wa mujibu wa kanuni, miogozo na sheria za maeneo ya kazi. Kufanya kazi kwa misingi ya kanuni husaidia kupunguza migongano inayopelekea utendaji mbovu. Ni vigumu kufanya kzai kwa mujibu wa sheria, lakini inawezekana kupunguza uwezekano wa migawanyiko na makundi yanayofanya utendaji wa mtu kushuka na hatimaye kuondolewa kazini.

Monday, June 11, 2012

MBINU ZA KUWINDA AJIRA (2)

3. VYANZO VYA MAARIFA
Ili kupata kazi, mtu anapaswa kuwa tofauti na waombaji wengine wote. Ili kuwa tofauti, pamoja na mambo mengine, maarifa ni kitu muhimu. Kuna vyanzo vitatu vya maarifa:

3 (a) Elimu ya Darasani.
Hii ni elimu mtu aipatayo kutoka kwa Wakufunzi rasmi, katika mazingira ya shule; elimu itolewayo katika mfumo rasmi wa elimu. Kwa mfano, Sekondari, Vyuo vya Ufundi n.k. Elimu hii ni ya kufuta ujinga, kwani inao mchango kidogo sana katika kufanikiwa kwa mtu.

3 (b) Elimu ya mitaani.
Hii ni elimu itoknayo na mwingiliano wa mtu na jamii anayoishi. Kwa mfano; kuhudhuria makongamano, kuwasikiliza watu waliofanikiwa, kufanya majadiliano n.k. Elimu hii humpa mtu maarifa sahihi ya kukusanya na kutumia rasilimali zinazomzunguka kwa ufasaha zaidi. Elimu hii ndio iliyowawezesha watu wengi kupata mafanikio.

3 (c) Elimu ya vitabuni.
Elimu hii hutokana na kusoma vitabu vyenye mlengo chanya. Vitabu vinamwezesha mtu kupata mawazo na ushauri kutoka kwa watu maarufu na waliofanikiwa; ambapo isingelikuwa watu hao waliweka mawazo yao katika vitabu, ingekuwa vigumu sana hata kusalimiana nao.

Kupitia vitabu, mtu anapata kujua watu maarufu walifanikiwaje kufanya biashara, kuajiriwa, kuongoza n.k, hivyo na yeye achukue uamuzi gani kulingana na hali inayomsonga.
vyanzo vote ni bora; ila Elimu ya darasani na elimu ya mitaani ni vyanzo sahihi zaidi vya maarifa, kwani ni vya urahisi na uhakika, na vinaelezea hali halisi ya maisha.

4. KUFAHAMU MAHITAJI YA MWAJIRI.

Kabla ya kwenda kuomba kazi kwenye taasisi au shirika (ikiwa kama kazi haikutangazwa), mtu anaweza kufanya uchunguzi juu ya ndoto, mikakati na changamoto zinazoikumba taasisi husika. Kila mwajiri anatafuta:

4 (a) Mtu atakayeongeza thamani kwenye kampuni..
Waajiri hutafuta mfanyakazi atakayeongeza ubora wa huduma au bidhaa huku akipunguza changamoto zinazoikabili kampuni. Waajiri wanataka watu waoweza kuiokoa kampuni isiangukie kwenye msukosuko wa kiuchumi.

Linapokuja suala la kuomba kazi, Watanzania wanamatizo makuu matano nayo:
¤ uwezo mdogo wa kuongea na kuandika lugha ya Kiingereza, kwani Kiingereza ndio lugha inayowaunganisha watu wengi;
¤ kutojiamini, Watanzania wengi hawawezi kutetea kile wanachokiamini kuwa ni sahihi hasa baada ya kupewa changamoto;
¤ kutoa huduma mbaya kwa wateja, kukosa kujua na kumudu mbinu za kuwahudumia wateja hufanya biashara nyingi kufilisika;
¤ kushindwa kujiwasilisha; watu wengi hawajui wavae nini, watembeeje, waongee nini na wapi n.k. Hili ni tatizo kubwa hata kwa viongozi;
¤ uwezo mdogo wa kutumia vifaa pamoja na sayansi na teknolojia. Takribani 3% ya Watanzania ndio wanaoweza kutumia huduma za mtandao wa Intaneti kama; barua pepe, nukushi, Facebook, Twitter, YouTube n.k

4 (b) Watu halisia.
Waajiri hawataki ubora wa vyeti au watu wanaoweza kujieleza bila ya matendo, bali watu wachapa kazi.
Waajiri hawataki watu wenye mipango anuwai, bali mipango inayotekelezeka.
Itaendelea.....

Monday, June 4, 2012

MBINU ZA KUWINDA AJIRA (1)

Changamoto ya ukosefu wa ajira ni kubwa, si kwa Tanzania tu bali hata kwa mataifa mengine. Takribani kila Taifa kuna idadi kubwa ya watu wanaopunguzwa kazini kutokana na mabadiliko ya teknolojia au ili kumudu gharama za uendeshaji, pia kuna wahitimu wengi kutoka vyuoni.

Hatari kubwa ni kwa wahitimu kutoka vyuoni kwa kuwa waajiri mengi humtaka mwajiriwa mtarajiwa awe na uzoefu wa miaka kadhaa katika kazi anayotaka kuomba.
Hivyo wahitimu wanapaswa kufanya kazi ya ziada kwani santuli (CV) zao hazina thamani, zote zinafanana.

Kutokana na kufanana kwa CV, mhitimu anapaswa kuhakikisha anajiuza, si kutegemea CV impatie kazi.
Mtihitimu anaweza kuijuza kupitia: (i) muonekano wake (ii) vionjo alivyo navyo (iii) hamasa na (iv) imani aliyo nayo juu ya kufanikiwa. Pia mtu anapaswa kuishi kadiri ya fani yake kama: kuvaa mavazi ya heshima, kuongea kwa ufasaha, kutekeleza majukumu (kuacha uvivu) n.k. Vitu hivyo ni bora zaidi ya elimu ya darasani.

2.0. MIKAKATI

2.1. Kuwa na Lengo.
Soko la ajira ni ngumu, pia linabadilika badilika kila wakati. Watu wanaohitaji kazi ni wengi kuliko nafasi zinazotolewa na soko la ajira.

Hivyo mtu yeyote anayetafuta kazi lazima awe na LENGO mahususi. Watu wengi, hata wasomi wa vyuo vikuu hawana malengo. Wahitimu wengi huwa wamejiandaa kitaaluma tu! Hawajiandai ili kupata misingi ya kukabiliana na changamoto maishani. Hivyo kupata changamoto nyingi katika kujikwamua kimaisha.

Katika mchakato mzima wa kazi, kuna makundi matatu ya watu; washindi, washindi wasiojitambua na wasiojitambua.

i) Washindi.
Watu hawa hupata kazi wanayoitaka, kipato wanachotaka na kufanya kazi katika mazingira wanayotaka. Watu hawa ni majasiri (hujiamini), hutumia rasilimali zao kwa makini, wapo tayari kumfuata mtu mwenye madaraka (mf Mkurugenzi) yeyote na kumweleza malengo na changamoto zao. Watu hawa nui wachache sana.

ii) Washindi wasiojitambua.
Watu hawa wana dhamira ya dhati ya kupata na kufanya kazi, wanatumia jitihada zao, wanajiamini kidogo (ni waoga), hutegemea kupata kazi zinazotangazwa magazetini n.k. Huwa hawapati kazi kwa haraka kwa kuwa hawapo tayari kusimamia malengo yao, pia hawaelekezi nguvu zao kwa makini.

iii) Wasiojitambua.
Watu hawa hawajui ya kwamba hawajui, yawezekana wamesoma, lakini hawajitambui; elimu yao hijawakomboa. Huwa wanaishi bora mradi wakiamini kupata kazi ni bahati, na bahati yao haijaifika. Ni waoga kupindukia. Humtegemea Mungu kwa kila jambo hata kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wao.
KUPATA KAZI KUNATAKA KUFAHAMIKA ZAIDI YA KUWA NA UWEZO WA DARASANI. Itaendelea......

Monday, May 28, 2012

FAIDA ZA KUTAFAAKARI JUU YA KIFO

Kwa mtu kuamua kuwaza juu ya kifo chake ni jambo zuri, tafiti zimethibitisha hivyo tofauti na mitizamo ya watu.
Watu wengi huogopa sana pindi wanapoona jeneza au kupita makaburini au kusikia juu ya msiba. Hivyo kujikuta wakitafakari juu ya maisha yao.

Kuna baadhi ya mitizamo hasi ya kwamba mtu anayetafakari juu ya hatima yake, na kuongea hakawii muda mrefu bila ya kufariki. Baadhi ya watu huenda mbali zaidi na kusema ya kwamba mtu anayekaribia kufa huona baadhi ya dalili ndani ya siku arobaini kabla ya kifo chake, hivyo kumfanya aongelee kufa.

Kuna faida nyingi sana kwa mtu anayamua kutafakari kwa kina juu ya kifo chake na jinsi mambo yatakavyokuwa baada ya kifo chake. Miongoni mwa faida hizo ni:

a) Kumfanya mtu ajione sawa na wengine.

Watu wenye mali nyingi, hadhi n.k hujisahau. Pindi wanapohudhuria misiba hupata nafasi ya kujishusha, hivyo kujiona hawana tofauti kubwa na wale wanaowazika, kwani hao wanaowazika hawakupenda kufa, pia wao hawajui kwa nini wapo hai na watakufa lini. Hivyo kuimarisha uhusiano baina yao na jamii.

Pia kwenye ibada za mazishi viongozi wa dini hupata wakati wa kuhamasisha watu waishi kwa upendo ili apate mapumziko mema baada ya maisha ya duniani.

b) Kusaidia kuimarisha afya.

Watu hukata shauri na kwenda hosptali au vituo vya afya ili kupata kuchunguzwa afya zao (mfano kupima VVU, malaria n.k) baada ya kuambiwa madhara ya matendo yao au hatari zinazowasonga, kiasi cha kutishia uhai wao.

Pia watu huchukua tahadhari kama kufanya mazoezi, kubadili mfumo wa vyakula n.k ili kupunguza uwezekano wa kupata matatizo kama shinikizo la damu, kisukari n.k.

c) Kuandika mirathi.
Kuwaza juu ya kufa humfanya mtu kuandika mirathi au kuweka utaratibu mzuri wa ugawanyaji wa mali anazomiliki.

Pia huwafanya wazazi kuwajengea watoto wao misingi ya utunzaji na ukuzaji wa mali za familia, hususani kwa familia au watu wasio na uwazi kwa watoto au ndugu zao juu ya idadi na ubora wa mali wanazomiliki.

Kila nafsi itaonja mauti! Hivyo kila mtu anapaswa kutafakazi, je matendo yake yanashabihiana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu?

Wakati wa kurudi kwa Muumba hakuna nafasi ya kubeba hata sehemu kidogo ya mali mtu alizozalisha au kwa mabavu au kwa njia njema. Kila mtu anapaswa kuwa mfumo wake wa maisha utakaodumu hata baada ya kifo chake. Kwani mtu hufa lakini matendo na mwenendo wake mwema humweka hai na kubaki kama ua katika jamii alimoishi.

Monday, May 21, 2012

KANUNI ZA KUKUZA MALI

Kuna kanuni kuu nne zinazomwezesha mtu kupata mali au pesa, kuweza kuwa na uhakika wa kipato kwa muda mrefu katika kila uwekezaji.
Kanuni hizo ni kanuni ya mapato, kanuni ya matumizi, kanuni ya kuweka akiba na kanuni ya uwekezaji uchambuzi wa kanuni hizo ni kama ifuatavyo:

1. Kanuni ya mapato.

Kila aina ya kipato (iwe pesa au mali) hutengenezwa kwanza katika fikra.
Ili kupata kila kitu kunahitajika mbadilishano wa mawazo baina ya mtu na mtu au baina ya mtu na mazingira.

Kuna njia nyingi za kupata kipato au rasilimali yoyote ile. Miongoni mwa njia hizo ni; kuomba kutoka katika taasisi za fedha kama benki, kuomba msaada kutoka kwa ndugu au jamaa, kudunduliliza kidogo kidogo, kuomba msaada kutoka katika taasisi zinazokuza uwezo wa makundi ya watu kama vijana, wajane n.k

Ukubwa au ubora wa kipato hutegemea ubora wa mawazo na kiasi cha ushawishi alicho nacho mtu. Ikumbukwa ya kwamba si rahisi kwa mtu kuchangia kwa hali au mali juu ya kumwezesha mtu mwingine, hususani asiye na uhusiano naye.

2. Kanuni ya matumizi.

Bila ya matumizi hakuna mapato. Hakuna cha bure kamwe! Kuna aina kuu mbili za matumizi, nazo ni matumizi ya kawaida na matumizi ya uzalishaji (uwekezaji).

Matumizi ya kawaida ni matumizi yote yasiyolenga kuongeza kipato (mtaji) hata kidogo. Matumizi hayo ni kama kununua nguo, chakula, vinywaji na vitu vyote vinavyohisana na kukidhi mahitaji ya mara kwa mara ya binadamu.

Aina ya pili ya matumizi ni matumizi ya uwekezaji (kukuza kipato). Haya ni matumizi yote yanayohusiana na kuongeza (kuzalisha) mali; kuzalisha mali iwe kwa muda mfupi au mrefu. Matumizi haya ni kama; kununua hisa, kununua bidhaa ili kuuza, gharama za kulima au kufuga ili kuuza n.k

3. Kanuni ya kuweka akiba.

"Matumizi bila akiba, pesa zitatukimbia", pia haba na haba hujaza kibaba. Kwa baadhi ya watu walio wengi suala la kuweka akiba ni ngumu sana. Ugumu huo hujidhihirisha pale mtu 'anapokula mpaka mbegu'.

Watu wengi na mbao ni masikini hawatoweza kupata mafanikio endelevu kwa kuwa hutumia pesa au rasilimali nyinginezo bila ya kufikiri kesho itakuwaje. Humwachia Mungu kila jambo, hata yale mambo ambayo Mungu aliyowapa mamlaka na uwezo wa kuyatatua.

Ili kupata na kutunza mtaji mtu anapaswa kutunza kati ya 25% na 30% ya kipato chake chote, hususani pesa au bidhaa zinazoweza kubadilishwa na pesa kwa urahisi.

Utaratibu wa kutunza (kuweka akiba) humfanya mtu kuwa na nidhamu juu ya kila rasilimali anayoipata. Kuwa na akiba pia humfanya mtu kuwa na utulivu na kufikiri zaidi juu ya kuimarisha kile alichokipata. Kuweka akiba huwa ngumu kwa baadhi ya watu kwa kuwa hawana MALENGO.

4. Kanuni ya uwekezaji.

Tumia pesa zikuzoee, na pesa huzaa pesa ni baadhi ya sentensi chache zinazoweza kueleza dhana mzima ya uwekezaji kama mhimili wa nne wa utajiri.

Uwekezaji huja baada ya kuweka malengo na kukusanya pesa au rasilimali kwa ajili ya lengo husika. Matumizi kwa ajili ya uwekezaji yanapaswa kuelekezwa kwenye lengo husika na kwa makini ili kuhakikisha hakuna ufujaji wa mali.

Ili kuwa makini katika matumizi ya uwekezaji, mtu anapaswa kujiuliza, je natumiaje rasilimali zangu sasa hivi ikilinganishwa na lengo husika?

Watu hupata faida kidogo au isiyoridhisha kwa kuwa; wanaogopa kuwekeza katika miradi inayochukua muda mrefu ili kupata faida au hawana mitaji, au huwekeza kwa kufuata mkumbo n.k. Hivyo watu wengi wakigombania fursa chache za kuwekeza na hivyo kusababisha ukosefu wa soko kwa bidhaa walizozalisha.

Kunahitajika kufanya kazi kufa au kupona ili kuhakikisha uwekezaji unazaa matunda yaliyokusudiwa.
HAKUNA ALIYEZALIWA AKIWA TAJIRI, KILA MTU HUSUSANI MIMI NINANAWEZA KUWA TAJIRI.

Monday, May 14, 2012

KUMUDU UVUMILIVU

Mafanikio yoyote yale huja baada ya uvumilivu, kwani hakuna cha bure, pia bure ni ghali. Si rahisi kumudu changamoto na hata kufikia mafanikio, bila ya kuwa na zana sahihi.
Miongoni mwa zana zitumikazo ni zifuatazo:

a) Kuwa na hamu.

Kumudu makali ya changamoto huweza kufanikiwa ikiwa mtu husika anayo hamu kutoka moyoni, kuwa na hamu ya mafanikio husika; anayo dhamira ya dhati itokayo katikati ya moyo wake, wala si itikadi za watu wakaribu. Hamu ya mafanikio hujijenga katika akili, kisha kumpa mtu husika sababu za kusonga mbele; kusonga mbele ili kukabili kile kinacho waangusha wengi.

Kwa mfano; jinsi atakavyosherekea kuhitimu masomo, jinsi atavyoweza kuonyesha kwa matendo ya kuwa hakuna lisilowezekana, tafrija ya kuwa na makazi ya kudumu n.k.

b) Kuchambua mikakati.

Ili kukabiliana na changamoto, mtu husika anapaswa kuchambua kwa makini mikakati (njia) anayotarajia kupita au kutumia.

Uchambuzi wa kina juu kila hatua, na ambao utahusisha vikwazo vya hatua husika humsaidia mtu kuona kwa ufasaha ni nini cha kufanya wakati gani, kwa nini na jinsi ya kukabili vikwazo vitokanavyo. Kwa mfano; ili kuanzisha kilimo mtu anapaswa kujua; sababu ya yeye kulima, mahitaji ya kilimo kwa ujumla, mahitaji ya zao husika, soko la zao husika n.k

c) Kuchukua hatua.

Watu wengi sana huwa na mikakati mizuri sana, bali hushindwa kuitekeleza kwa kuwa hawachukui hatua kwa wakati sahihi. Watu huogopa kuchukua hatua ili kukabili changamoto ingali bado ndogo, hatimaye kuwaangusha nyakati za baadaye.

Waswahili wanasema 'nyani akinyeshewa na mvua husema, nitajenga nyumba kesho' na kesho haitokei. Mtu asijipangie majukumu makubwa ndani ya muda mfupi. Kumbuka, mdogo mdogo ndio mwendo.

d) Kuhusiana na watu sahihi.

Kuwa na marafiki ambao hutia moyo; ambao wamefanikiwa; ambao wanayo ndoto ya dhati ya kufanikiwa husaidia kupata msaada wa hali au mali pindi changamoto zinapajitokeza.
Imeandikwa, "chagua mazingira sahihi kwa kuwa yatakuumba, chagua marafiki sahihi kwa kuwa utafanana nao".

e) Kuamini hakuna kushindwa.

Changamoto zinapaozidi haziashirii kushindwa, bali zinaashiria au mtu hakuchukua juhudi sahihi au hakuchukua njia sahihi, au ni hali ya kawaida ambayo lazima mwana-harakati yeyote aipitie.

Mtu asiangalie ni mara ngapi ameanguka, bali aangalie ni mara ngapi amesimama na kusonga mbele. Pia ifahamike kwamba maisha si lelemama.

f) Kuamini hakuna cha bure.

Katika ulimwengu huu wa utandawazi; ulimwengu wa ubepari; ulimwengu ambao kila kinachofanywa popote pale kinatarajiwa kuleta mapato; kila maamuzi yanahusisha madhara ya kiuchumi au kwa mtu au kwa taasisi au kwa Taifa husika. Hakuna fursa ya bure kamwe!

Kila mtu, taasisi au taifa hupigana ili kupata mafanikio, hivyo mgongano wa kimaslahi ni lazima utokee. Hakuna aliye tayari kutumia gharama zake ili kumshibisha mtu mwingine bure.
Mfano, kutokana na uhaba wa maeneo ya kufanyia biashara, mtu yupo tayari kutoa msaada ili iwe rahisi kushawishi na kununua eneo la biashara kwa bei nafuu sana.
NYANI MZEE AMEKWEPA MISHALE MINGI, VIVYO HIVYO, MTU MWENYE MAFANIKIO AMESHINDA CHANGAMOTO NYINGI.

Monday, May 7, 2012

UVUMILIVU

Waswahili wanasema "MVUMILIVU HULA MBIVU". Ikiwa kama mtu atavumilia kutenda yaliyo sahihi, mahali sahihi, kwa watu sahihi na kwa muda sahihi atapata matokeo sahihi.

Uvumilivu ni hali ya kutia juhudi kwa kile mtu anachoamini kitampa mafanikio chanya. Imani humpa mtu uvumilivu na kisha uwezo katika harakati za kutimiza malengo.

Ikiwa kama mtu hakupata matokeo chanya au matokeo hayakumridhisha, anapaswa kuangalia upya mbinu alizotumia na kisha kujaribu tena; kurudia kwa mbinu nyingine.
Kumbuka: baada ya taabu - faraja; na uchungu ukizidi ndipo kujifungua kunakaribia.

Imebainika kwamba, ikiwa mtu atakuwa katika mwenendo usiofaa kwa muda mrefu, mtu huyo hubadili mwenendo na kuwa mtu mwema, ikiwa tu kama alitia juhudi katika kubadili mwenendo.

Uvumilivu hutiwa chachu kwa maneno matatu ambayo ni; NINAWEZA, NITAWEZA na LAZIMA.

Uvumilivu huonyesha dhamira ya kushinda. Dhamira ya kushinda hutegemea mtizamo wa mtu ambao ni; ninaweza, nitaweza na ni lazima kufanya kitu fulani ili kuboresha maisha.

Ikiwa kama mtu atakumbana na changamoto (wakati mgumu), kana kwamba ikaonekana hawezi kupiga hata hatua moja kuelekea mbele, asikate tamaa, kwani baada ya mawimbi makali hali ya bahari huwa shwari, na pia mawimbi hayadumu milele.

Watu wanaovumilia huku wakitia juhudi hupata mafanikio pale ambapo wengi hushindiwa. Mtafutaji hachoki, anayechoka hatofanikiwa kamwe!.

Mtu anapasa kutumia mawe (changamoto) yaliyopo njiani ili kuimarisha msingi; ili kutengeneza nafasi za kufanikiwa. Mawe wanayoyakataa waashi ndio huwa mawe makuu ya pembeni.

Bila ya kupambana hakuna ukuaji; kama hakuna ukuaji hakuna ushindi. Tunu huimarishwa na uvumilivu unaoakisi matunda ya jitida husika.

Changamoto kubwa ya kukosa uvumilivu ni; kuogopa lawama, kuogopa kushindwa na kutochukua hatua sahihi kwa wakati sahihi.

Monday, April 30, 2012

MBINU ZA KUKUZA MAHUSIANO BAINA YA WATU

Mahusiano baina ya mtu na jamii yake ndiyo yanayomfanya mtu au afanikiwe au asifikiwe. Mahusiano baina ya mtu na mtu hutegemea uwezo wa mtu husika kushirikiana na jamii yake, kushikiana kunakojengwa na kutegemeana; na si kutegemea.

Ili kuboresha mahusiano, yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:-

a) Upendo.
Ili mtu apendwe anapaswa kujipenda kwanza; kujipenda huanza kwa muonekano wa ndani na kisha wa nje. Kujipenda na kuwapenda watu wengine huonekana machoni mwa watu kupitia mienendo. Mtu anayewapenda wenzake hujitahidi kutoa msaada wa hali au mali ili wenzake watimize malengo yao.

b) Kukumbuka majina.
Mtu anapowaja watu anaowasiliana nao kwa majina. Au kuwaeleza jinsi anavyojua kule watokako huwatia watu faraja, kuwafanya wote wajione ni jamii moja. Pia huwafanya watu husika kujiona ni muhimu (wana thamiwa) miongoni mwa jamii.

c) Kukubali juhudi za watu.
Kukubali matunda (matokeo) ya kazi za watu wengine; kwa kuzipa thamani au ubora unaotakiwa hudhihirisha harakati za watu na kuwafanya waongeze matumaini na juhudi.

d) Kusikiliza kwa makini.
Kusikiliza ni bora zaidi ya kuongea katika nyakati nyingi. Mtu hudhihirisha jinsi gani habari yake inavyoungwa mkono kwa kadiri anavyosikilizwa. Hivyo kukuza hekima na uelewa wa msikilizaji. Baada ya kusiliza, mtu anapaswa kujibu kadiri ya busara na dhamira yake.

e) Kuruhusu hisia za watu.
Kuruhusu hisia, mtizamo, au mada kutoka kwa mtu/watu zijadiliwe humfanya mtu/watu kuzungumza kwa uhuru juu ya kufanikiwa na changamoto zao. Hivyo kumfanya mtu/ watu kufurahia uhusiano wao na jamii yao.

f) Kutia moyo.
Kuwatia moyo watu ambao hawakufanikiwa kiasi cha kuridhisha hutoa ahueni kwa mhanga. Yafaa kuwatendea watu kadiri ya mtu anavyotaka atendewe na wenzake. Kuwatakia watu heri husaidia kuepuka mawazo au kauli za kuwarudisha nyuma.

Thursday, April 26, 2012

KUFANIKISHA MAKUZI YA WATOTO KWA MZAZI MMOJA

Katika nyakati hizi, familia zilizochini ya uangalizi wa mzazi mmoja, hususani mama, zimeongezeka sana hata kufikia idadi sawa au zaidi ya familia zenye baba na mama katika jamii nyingi.
Kuna sababu nyingi zinazopelekea hali hii kama; kifo, utelekezwaji wa familia, kuhamishwa kikazi, masomo hususani elimu ya juu n.k

Changamoto zinazoambatana na malezi ya mzazi mmoja ni nyingi, ikiwamo; ufinyu wa kipato, kukosa ushirikiano kutoka kwa mzazi wa kufikia, upweke unaopelekea msongo mawazo n.k

Kukabili Jukumu.

Jukumu gumu katika malezi ni kelea mtoto/ watoto wachanga. Watoto wadogo wanahitaji uangalizi wa karibu. Hata hivyo jukumu hilo kubwa la malezi linaweza kupunguzwa kwa:

a) Kutafuta msaada.
Kutafuta msaada ni muhimu sana, hata kama mzazi husika anahisi ataweza kulea akiwa peke yake. Ni vigumu sana kulea mtoto bila msaada. Msaada unaweza kuombwa kutoka kwa ndugu, jirani, rafiki au mashirika yanayohusika na kulea watoto. Ikiwa kipato cha mzazi kinaruhusu mzazi anaweza kumwajiri yaya.

b) Kuweka mipango.
Mzazi anapaswa kupanga ratiba na kuhakikisha anaitekeleza. Watoto huwa na amani ikiwa wanajua saa ambayo baba/ mama atakayorudi. Pia ikiwa wanaona juhudi za mzazi katika kuwalea.

c) Kujibu maswali ya watoto.
Watoto huuliza maswali magumu sana, kwa kuwa watoto hupenda kudadisi juu ya yale wanayoyasikia. Watoto huuliza maswali juu ya baba/ mama ambaye hayupo. Mzazi husika hapaswi hata kidogo kupuuza maswali kutoka kwa watoto, bali atoe majibu sahihi na yenye ufafanuzi katika hali ya upole na unyenyekevu.

d) Kuzingatia maadili.
Mzazi anapaswa kuweka sheria na kanuni chache na zinazotekelezeka. Hii itawasaidia watoto kujiwekea mipaka maishani. Watoto wafundishwe kufanya kazi kwa ushirikiano tangu wakiwa wadogo. Mzazi awe na kiasi katika kutoa kazi na adhabu. Pia mzazi awaambie wasaidizi wake, juu ya matarajio yake kwa watoto wake.

e) Kuweka vipaumbele.
Ufinyu wa bajeti ni kikwazo kikubwa kwa familia ya mzazi mmoja. Mzazi anapaswa kuweka bajeti kadiri ya kipato chake. Ili kuepuka mzigo wa madeni, mzazi anapaswa kuepuka anasa. Pia mzazi awaambie watoto sababu za mapendekezo yao kutotekelezeka.

f) Kukaa na watoto.
Watoto huwa na furaha na amani ikiwa watakuwa na mahusiano mazuri na ya karibu baina yao na mzazi wao. Mzazi ahakikishe anapata muda kwa ajili ya kuongea, kusoma, kutembea, kuimba n.k na watoto. Mzazi asiruhusu watoto kuangalia TV kwa muda mwigi, hususani vipindi visivyo na umuhimu kwa watoto. Kufanya hivyo huimarisha familia.

g) Kujijali.
Mzazi ahakikishe anajali afya yake, kazi yake, jamii yake n.k. Kufanya hivyo kutasaidia kukuza ustawi wa roho na mwili. Mzazi atenge muda wa kupumzika na kuwasiliana na wadau wanaomsaidia katika malezi. Mzazi husika anapaswa kuchunga afya yake kwani, kama ikiwa ataugua hali ya familia itakuwa matatani.

Monday, April 9, 2012

MISINGI YA THAMANI YA MTU

Kila anachofanya mtu maishani au kuongea kinaakisi jinsi mtu anavyohisi, kile anachotamani, kile anachoamini ni stahili yake na jinsi gani anajali thamani yake popote pale alipo.
Kupata bahati, kuungwa mkono, kupata changamoto n.k ni matokeo ya jumbe zinazotolewa na mtu husika.

Thamani ya mtu inajengwa na mtu mwenyewe pale awapo; iwe kazini, kitaaluma, n.k. Ili kukuza na kuimarisha thamani ya mtu, yafuatayo ni muhimu:

1. Kujiheshimu.
Mtu anapaswa kujiheshimu (kuwa na adabu). Kujiheshimu kunahusisha akili, mwili na nafsi. Kujiheshimu hujidhihirisha jinsi mtu anavyovaa, anavyotembea, anavyowasiliana, anavyopanga mambo ya siku kwa siku n.k

2. Kujisafisha.
Mtu anapaswa kuwa na nafsi inayobubujika kama chemchemu. Nafsi ya mtu inapaswa kububujika upendo; upendo utakaomweka mtu mbali na chuki, kisasi n.k. Upendo ndio unamfanya mtu aombe msamaha kwa dhati na kujutia mabaya aliyowafanyia wenzake.

3. Kujipenda.
Kiungo muhimu katika ustawi wa mtu ni kujipenda. Watu wanaojipenda huwa na fikra na nyoyo nyepesi; huwaza chanya na kuvuta bahati.

Kujipenda na kutambua thamani yake humfanya mtu kufikiri madhara ya matendo yake na kuchukukua hatua stahiki. Kujitambua ndiko kunakomfanya mtu kuwaza madhara ya vipodozi, kukuza viungo, ulevi wa kupindukia, kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa n.k.

4. Kuchuja mawazo.
Mtu hujengwa na mawazo; mtu huishi kadiri awazavyo. Kitu kinachowatofautisha watu ni jinsi wanavyochuja na kufanyia kazi mawazo wanayoyapata kupitia milango ya fahamu.

Mtu hutenda mabaya ikiwa aliruhusu na kuhifadhi mawzo mabaya, vivyo hivyo, mtu hutenda mema ikiwa aliruhusu, kuhifadhi na kuchambua mawazo kwa mtizamo chanya.

5. Kuwasoma watu.
Njia bora ya kupata mafanikio ni kusoma kutoka kwa watu; kusoma jinsi watu walivyofanikisha mafanikio na thamani yao; jinsi walivyozishinda changamoto.
Mtu anapaswa kuwatafuta na kuwa karibu na watu wanaojiamini; kuwasikiliza (kusoma maandiko yao) na kufuatilia jinsi wanavyotenda.

6. Kuchagua vishawishi.
Ni muhumu sana kwa mtu kuwa makini na kile kinachomfanya achukue aina fulani ya maamuzi. Mtu anapaswa kuruhusu vishawishi vinavyompelekea kufanya maamuzi yanayojenga na si kubomoa.

Vishawishi vinaweza kuwa kauli za watu, mienendo ya watu n.k. Vishawishi vinapaswa kusaidia kuondoa au kupunguza changamoto za kimaisha kwa mtu au jamii husika.

7. Kuepuka mizani.
Mtu anapaswa kuwa makini sana pale anapo-oanisha mafanikio yake na ya mtu mwingine. Ni bora kujipima kupitia malengo; japo jamii haiwezi kufanya hivyo. Mara nyingi watu wanaolinganisha mafanikio yao na yale ya wengine huishia kukwazika na kujishusha thamani yao.

Mafanikio ya mtu si mizani sahihi kwa kuwa mtu (mizani) husika anaweza kupata mafanikio haraka kupitia misaada, bahati, kupata changamoto nyepesi n.k

Monday, March 26, 2012

JE PESA NI KILA KITU?

Je ili kupata takribani kila kitu mtu anachotaka, ianampasa mtu kuwa na pesa? Jibu ni NDIO, na hiyo ndio sababu inayowafanya watu watafute pesa kila wakati; iwe usiku au mchana. Watu wamepewa majina mengi kama; mafisadi, wezi wa kalamu, matapeli, n.k kutokana na harakati zao za kusaka pesa. Huku pesa ikipewa majina kama; mkwanja, mapene, mawe, noti...

Kutafuta na kumiliki pesa nyingi ndi
o lengo la watu wengi. Hii haibadili ukweli kwamba watu hawapati pesa za kutosha kukidhi mahitaji yao; hata ya kila siku. Ikiwa pesa hazitoshi, je ni lazima kutafuta pesa?

Ukiwaza kwa kina utagundua kwamba, hakuna binadamu anayetaka pesa. Watu wanataka bidhaa au huduma, na wala si pesa. Hivyo, watu wanatafuta pesa ili kununua bidhaa au huduma kwa ajili ya kukidhi mahitaji; ili kukidhi mahitaji yasiyokwisha.

Kuelekeza mawazo na jitihada nyingi katika kutafuta pesa kumewafanya watu wasitafute njia mbadala za kukidhi mahitaji yao. Watu wanaamini pesa ndio kila kitu, hata wanasahau sababu za kutafuta pesa. Kuna baadhi ya watu wanatafuta pesa ili kuwa na 'usalama' na furaha, vitu ambavyo haviitaji pesa.

Kutaka pesa nyingi kumewafanya watu kuwa watumwa wa pesa, kumewafanya watu wachague au waache fani zao za awali na kukimbilia kwenye fani zenye uhakika wa pesa nyingi ili kununua furaha, bila ya kujali hatari (athari) zinazohusiana na fani husika.

Takribani watu wote maarufu na waliofanikiwa walielekeza nguvu zao kulinganana na vionjo (hobby) vyao, na wala si kufuta wingi wa fedha. Waliboresha vipaji vyao, na vipaji vyao viakawaletea pesa, heshima, furaha na usalama.

Ikiwa mtu anataka kupata mafanikio maishani, anapaswa kujiuliza; JE NINAHITAJI NINI HASA?
Ili kujibu swali hilo, mtu anapaswa kuandika vitu vyote anavyotaka kufanya au kuwa navyo bila ya kujali gharama. Wakati huo mtu husika akiwa mkweli dhidi ya nafsi yake; juu ya uhitaji wa bidhaa au huduma husika. Kisha mtu apitie tena orodha yake kwa kina huku akikadiria gharama.

Kwa kufanya hivyo kutamfanya mtu kutosema 'nahitaji maisha bora', bali atakuwa na malengo mahususi; kama nahitaji gari aina..., nahitaji nyumba iliyo na..., nahitaji elimu ya... n.k. Mtu atakuwa na malego ambayo, kama akielekeza nguvu ipasavyo, atakuwa na 'maisha bora'.

Kuwa malengo mahususi kunamfanya mtu kujua kiasi gani cha pesa anachohitaji, pia kujua mbinu mbadala anazohitaji ili kutimiza lengo husika.
Mbinu mbadala kwa kila jambo ni muhimu sana, kwani kuna baadhi ya mambo hayahitaji pesa, bali ufahamu, ushauri..... ambao unaletwa na mahusiano mazuri baina ya mtu na jamii yake.

Monday, March 19, 2012

KUUSHINDA WOGA ULIOPINDUKIA

Woga wa kupindukia (kupitiliza) ni hali ya mtu kuogopa na kujitenga na watu muda wote. Watu wenye woga wa kupindukia hukwepa kujihusisha na wageni n.k. Woga wa kupitiliza huwakosesha watu faida na nafasi za kujifunza kutoka kwa jamii yao.

Woga wa kupitiliza hujidhihirisha katika katika mazingira yafuatayo:
¤ Kukwepa mikutano.
Watu hawa hukwepa kadiri iwezekanavyo ili wasihudhurie mihadhara au sherehe za pamoja.
¤ Upweke.
Woga wa kupitiliza humfanya mtu atumie muda mwingi akiwa pekee (faragha), au kutoka jasho, kutetemeka n.k anapotakiwa kuzungumza hadharani.
¤ Kutowasiliana hadharani.
Woga wa kupindukia hupelekea mtu kupata kigugumizi, kutetemeka n.k wakati wa kuongea. Hali huwa mbaya pale mtu anapotakiwa kufafanua kwa umma jambo linalohusu utendaji kazi wa ofisi au kada yake.

Suluhu Dhidi ya Woga Uliopitiliza

Woga wa kupindukia unahusishwa sana na sababu za kibaiolojia (kurithi). Suluhu ipo ikiwa mtu ataamua kwa dhati. Zifuatazo ni baadhi ya mbinu zitumikazo:

1. Kutambua kiini.
Mwathirika anapaswa kutambua mazingira au hali inayopelekea woga. Kama chanzo cha woga ni kudai haki, mtu husika anaweza kutafakari madhara aliyopata yeye au jamii yake kwa yeye kukaa kimya.

2. Kuweka mkakati.
Baada ya kugundua kiini cha tatizo, mtu anapaswa kuweka mpango mkakati ili kuondoa tatizo. Mpango mkakati unaweza kuhusisha kubadili tabia, marafiki, maeneo ya kupumzika (vijiwe) n.k.

Kwa mfano, kama mtu anaogopa kujihusisha na jinsia tofauti, anaposwa kujihusisha na marafiki, ndugu n.k wenye ujasiri wa kuhoji bila kujali jinsia pinzani.

3. Kujipa changamoto.
Japokuwa ni ngumu kwa siku za awali, ili kupata mafanikio ya haraka, mtu anapaswa kujipa changamoto (mazoezi) kwa kufanya kazi inayomfanya mtu ahusiane mara kwa mara na watu wa aina mbalimbali.

Mtu anaweza kujitolea kwenye taasisi au shirika fulani kwa muda fulani.
Pia mtu anaweza kuongea bila ya kufikiri bila ya kufikiri mtu mwinine atajibu vipi? Mazoea humfanya mtu aondoe hofu.

JIPIME.
Jibu N kama jibu ni NDIO na H kama jibu ni HAPANA kwa maswali yafuatayo:

1. Je upo tayari kuzungumzia jambo linalokufurahisha katika kundi la marafiki zako?
2. Je unaweza kuanzisha mawaliano na mtu usiyemjua?
3. Je huwa unatetemeka, kutoka jasho au kupata mapigo ya moyo unapotakiwa kuongea hadharani?
4. Je mtu akitaja jina lako kwa sauti huwa unashtuka?
5. Je huwa huna raha ukiwa karibu na mtu wa jinsia tofauti, ambaye hujamzoea?
6. Je unaweza kurudisha mali yenye kasoro baada ya kununua?
7. Je huwa unashindwa kutetea hoja yako pale inapopata upinzani?
8. . Je mtu akikupita kwenye mstari wa huduma, unaweza kumwambia alivyofanya si halali?
9. Je huwa unalaumu pale mtu anapokuita (anapokupigia simu) wakati usio sahihi, kama usiku wa manane?
10. Je unaweza kudai salio (chenchi) pale muuzaji anapokupunguzia?
11. Je unaweza kukopa fedha ili kukamilisha manunuzi?
12. Je unaweza kukataa bidhaa pale mhudumu anapokuletea bidhaa ambayo hujaagiza?
13. Je huwa unajitenga katika mikusanyiko ili kukwepa malumbano?
14. Je kama mtu anavuta sigara hadharani, na moshi wa sigara unakukwaza, unaweza kumwambia?
15. Kama mchuuzi (mmachinga) akikuletea bidhaa nyumbani, eneo la kazi n.k huwa unanunua hata kama bidhaa husika haina umuhimu?

Ufafanuzi:
¤ kama majibu ya N ni kati ya 1 mpaka 5, hamna tatizo la woga
¤ kama majibu ya N ni kati ya 5 mpaka 10, kiwango cha woga ni wastani, japo ni muhimu kuchukua tahadhari.
¤ kama majibu ya N ni zaidi ya 10, kiwango cha woga ni cha hali ya juu. Mikakati madhubuti na ushauri utekelezwe haraka iwezekanavyo ili kupunguza madhara.

Monday, March 12, 2012

KUSHINDA HISIA ZA KUTOKUKUBALIKA

Kukataliwa ni hisia kali zinazomkabili mtu na kumfanya aamini hakubaliki miongoni mwa wengine. Hali hii inaweza kumkabili mtu kwa sababu za kijamii (tofauti ya rangi), migogoro ya kifamilia (hususani ya mahusiano), tofauti za kimtazamo, tofautu za kimadaraja (aliye nacho na asiye nacho) n.k

Hisia za kukataliwa, bila ya kujali kisababishi, hupelekea madhara makubwa kwa mtu husika kama:
¤ hupelekea ugomvi wa nafsi;
¤ kuvunja mahusiano baina ya mtu na jamii yake;
¤ kupunguza ufanisi kwa kushindwa kuelekeza nguvu kwenye kazi;
¤ kushuka kwa kinga ya mwili hivyo kupelekea maradhi ya mara kwa mara.

Jinsi ya Kuepuka Kukataliwa.
1. Kuzuia mawazo ya kukataliwa

Mtu anapaswa kukuza hisia (mawazo) chanya dhidi ya wengine, hususani wapinzani wake. Mikakati itumikayo ni kama; kutathmini sababu za kutokukubalika, kutathmini uhalisia wa mambo yanayoleta tofauti, kuamini kuna suluhu ya kudumu, n.k.

Mikakati hatarishi ni kama; kukataa kuwasiliana na mpinzani, kuamini 'mimi' ni sahihi, kuamini kwamba mtu husika hana bahati ya kukubaliwa, kukumbuka mabaya mtu aliyofanyiwa n.k

2. Kuepuka mazingira ya upweke.

Ikiwa baada ya ugomvi, mtu ataamua kukaa mazingira tulivu kwa muda mrefu, hupelekea chuki na kutaka kulipiza kisasi. Ili kuepuka upweke, mtu anapaswa kujihusisha na makundi ya watu (marafiki) ambao watatoa ushauri juu ya upatanisho.

3. Kujipa majukumu.

Mtu anapaswa kupanga majukumu ya siku kana kwamba siku nzima (na siku zote) inakuwa na majukumu. Majukumu yahusishe mawasiliano ya mara kwa mara baina ya mtu husika na wengine. Kuwa na muda siokuwa na matumizi huruhusu mtu kukumbuka maovu mtu aliyofanyiwa hapo awali.

4. Kusamehe na kusahau.

Mtu anapaswa kujitahidi kadiri ya nguvu zake zote kusamehe na kusahau maovu aliyofanyiwa na jamaa zake. Ikiwa kama mtu anataka kuishi kwa amani na upendo, kisha kukuza uhusiano anapaswa kusamehe kwa moyo wake wote makosa yote aliyowahi kufanyiwa.

5. Kutaka suluhu.

Baadhi ya watu husubiri upande wa upinzani uchukue hatua za kuleta suluhu. Hali huwa mbaya sana ikiwa kama kila upande utakaa kimya na kusubiri upande wa pili utake kurekebisha tofauti. Mtu anapaswa kujiuliza, je kukaa kimya huleta suluhu? Na je nitakaa kimya mpaka lini huku nikisubiri suluhu ije?

6. Kumsaidia mpinzani.

Ikiwa kama mtu ataamua kuchukua hatua na kubebe 'mzigo' unaomkabili mpinzani wake, atakuwa ameonyesha ubinadamu wa hali ya juu sana. Hivyo, mpinzani ataona hakuna haja ya kuendekeza vita. Kwani kana asingeekuwa mpinzani wake kutoa msaada wa hali au mali, basi angeweza kuangamia.

7. Kumwomba Mungu.

Ikiwa mtu anapata ugumu wa kusamehe na kusahau, kuanzisha mazungumzo ya upatanisho n.k anapaswa kumwomba Mungu kulingana na imani yake. Kumwomba Mungu husaidia kupata ujasiri utaovunja mizizi ya shetani. Kwani shetani hapendi amani miongoni mwa watu walio sura na mfano wa Mungu.

Monday, March 5, 2012

JINSI YA KUBANA MATUMIZI

Ubora wa matangazo, tabia ya mtu na kuwepo kwa bidhaa ndizo sababu zinazopelekea kuwepo kwa 'ulafi' nyakati hizi, hususani maeneo ya mijini.

Je kuwepo kwa bidhaa na huduma kwa wingi hupelekea furaha? Jibu ni HAPANA. Chunguzi zilizofanywa miongoni mwa vijana waishio miji mingi duniani, ikilinganishwa na wazee wao ambao hawakua na uwezo wa kumudu matumizi, zinaonyesha kwamba vijana wanayo furaha ndogo.

Je Jamii Itapata Faida Gani Ikiwa Itapunguza Matumizi?

1. Uhifadhi wa rasilimali. Rasilimali asilia zitatunzwa kwa kizazi kijacho ikiwa kutakuwa na matumizi endelevu ya huduma na bidhaa zitokanazo.
2. Mazingira safi. Uchafu utapunguzwa ikiwa kama kila mtu atatumia bidhaa na huduma kwa uangalifu.
3. Kukwepa mzigo wa madeni. Haitakuwa lazima kuchukua mkopo kila mara ili kugharamia matumizi ya kawaida. Hivyo, kupunguza utegemezi wa kifedha.
4. Kurahisisha maisha. Matumizi sahihi humfanya mtu ayaone maisha ni rahisi. Hivyo, kupunguza dhana ya maisha ni magumu katika fikra.

Mikakati ya Kupunguza Matumizi.

1. Kuweka vipaumbele.
Mtu anapaswa kuweka vipaumbele kulingana na matumizi ya fani, masomo, burudani n.k si kuyumbishwa na makundi. Vipaumbele viwekwe kwenye orodha kulingana na umuhimu wake.

2. Kuchambua matumizi.
Mtu anapaswa kufanya uchambuzi wa kina juu ya mahitaji ya wakati husika. Uchambuzi unaweza kufanywa kwa kujiuliza maswali kama; je ni lazima kununua bidhaa husika? Je hakuna mbadala wa bidhaa husika? Je kama nisingekuwa na fedha? n.k.

3. Kuwafikiria wengine.
Ni bora kununua bidhaa na huduma ambazo si tu zitamsaidia mnunuaji bali pia jamii ya wahitaji inayomzunguka kama; yatima, wajane, wazee, fukara n.k wanaomzunguka.

4. Kuepuka majina ya makampuni.
Yapasa kufanya uchambuzi kuhusu ubora na gharama, na si kununua bidhaa kwa kuwa imetengenezwa na kampuni fulani. Baadhi ya makampuni makubwa hutengeneza bidhaa hata zilizo chini ya kiwango, lakini hupata manunuzi makubwa kwa kuwa hufanikiwa kutangaza, kutoa punguzo la bei n.k

5. Kuahirisha matumizi.
Ni bora kusitisha ununuzi wa bidhaa au huduma isiyo na ulazima kwa siku, wiki au miezi kadhaa. Kusitisha manunuzi husaidia kufanya tafiti juu ya soko pia, husaidia kupunguza hamasa au ushabiki katika matumizi

6. Kupunguza matumizi ya kadi.
Mageuzi ya teknolojia yamewezesha watu kuwa karibu zaidi na fedha zinazohifadhiwa benki. Pia teknolojia imewezesha kufanya manunuzi kwa kutumia kadi za ATM.
Pia inashauriwa, kupunguza kiwango cha fedha za tahadhari mtu anazokuwa nazo popote aendapo.

7. Kuwalinda watoto.
Watoto ni sehemu kubwa sana ya jamii. Hivyo wanapaswa kusaidiwa kupunguza matumizi kwa:

(a) Kupunguza matumizi ya TV. Matangazo yanayoonekana kwenye TV huteka hisia za watoto. Hivyo, kuwafanya wanunue bidhaa hata bila ya wazazi/ walezi wao kujua.
(b) Kueleza ubaya wa matangazo. Watoto waelezwe ubaya wa kununua bidhaa kutokana na ushawishi wa matangazo.
MATUMIZI BILA AKIBA, FEDHA ZITATUKIMBIA..

Monday, February 27, 2012

KUTUNZA MGONJWA

Ni ukweli usiopingika ya kwamba, mgonjwa huwa na nafasi kubwa ya kupona au kupata nafuu haraka iwapo apata ushiriano wa kutosha kutoka kwa jamii inayomzunguka.

Pindi mtu anapofanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kugundulika kwamba anatatizo, taratibu za matibabu hufuata. Ikiwa mgonjwa atakosa ushirikiano kutoka kwa jamaa, rafiki, ndugu n.k zake hukumbwa na hofu, woga, mtizamo hasi n.k. Hivyo hupungua kinga ya mwili na hatimaye kupunguza uwezekano wa kupona kwa haraka.

Ikiwa mtu atathibitika ni mgonjwa, jamii inayomzunguka (muuguzaji) inapaswa kufanya yafuatayo ili kufanikisha uponyaji:

1. Kumsikiliza mgonjwa.

Si wagonjwa wote hupenda kuongea, ikiwa yupo, anapaswa kusikilizwa kwa makini na upendo. Ikiwa mgonjwa hapendi kuongea, yapaswa ajengewe mazingira ya upole na utulivu wa akili ili aongee kwa uwazi.

2. Kuongea juu ya ugonjwa.

Wakati muafaka ukifika, mazungumzo juu ya ugonjwa yanapaswa kufanyika. Mazungungumzo yanaweza kuhusu ukubwa wa ugonjwa katika jamii husika, dalili na matibabu. Mgonjwa anahitaji taarifa sahihi juu ya ugonjwa ili kujiandaa kiakili juu ya hatua zinazofuata. Pindi mgonjwa anapoomba maoni kutoka kwa mlezi, muuguzaji atumie busara ili kutomkwaza mgonjwa.

3. Kutodharau.

Ni kawaida kwa wagonjwa kulalamika, hata wengine kumlaumu daktari au Mungu. Katika hali hii, mgonjwa asijibu au kutoa ishara za dharau au kebehi. Muuguzaji ajitahidi kujua sababu za majibu au hisia za mgonjwa, huku akimfariji.

4. Kumsaidia mgonjwa kazi.

Iwapo mgonjwa anapenda kusoma, kuandika, kuangalia TV, n.k asaidiwe ili atimize azma yake haraka iwezekanavyo. Yote kwa yote, mgonjwa anapaswa kusaidiwa majukumu ya siku kwa siku kama vile kufua nguo, kunyoosha nguo n.k ili kufanikisha usafi na kumwondolea mawazo.

5. Kuwezesha mawasilaino.

Muuguzaji anapaswa kumuunganisha mgonjwa na rafiki au ndugu zake. Ili kufanikisha mawasiliano, muuguzaji anapaswa kutoa taarifa juu ya hali ya mgonjwa kwa watu wa karibu. Kutoa taarifa kunarahisisha mawasiliano, pia huwezesha upatikanaji wa misaada kwa haraka.

6. Kusimamia utekelezwaji wa magizo.

Muuguzaji anapaswa kupokea na kusimamia kwa makini maagizo kutoka kwa nesi au daktari. Muuguzaji anapaswa kusimamia maagizo juu ya utumiaji wa dawa, ufanyaji wa mazoezi (kutembea), huduma ya kwanza n.k. Ili kurahisisha utekelezwaji wa maagizo, muuguzaji anapaswa kutunza maagizo yote anayoambiwa na daktari au nesi. Ikibidi kuwe na mawasiliano (simu) baina ya muuguzaji na Muuguzi.

Pia ni vizuri kumuomba Mungu kwa pamoja (mgonjwa na muuguzaji) kwani tafiti zimethibitisha kwamba wagonjwa hupata faraja na kupata nafuu/ kupona haraka pale sala zinapofanyika, sala za kuwaombea wapone haraka.
Neno muuguzaji linawakilisha mtu au watu wanaomhudumia mgonjwa siku kwa siku (iwe nyumbani au hosptali), na wala si Nesi.

Monday, February 20, 2012

JINSI YA KUEPUKA MADHARA YA TABIA HATARISHI

Kuna watu wengi waliyomo hatarini kutokana na mienendo yao mibaya. Watu wengi hususani vijana wamo hatarini kutokana na kunywa pombe kupita kiasi, kuvuta sigara, kufanya ngono kiholele, kutumia madawa ya kulevya n.k

Watu hawa wanafahamu wanayoyafanya ni hatari kwao na kwa jamii yao. Ni hatari kwao kwa kuwa huhatarisha afya zao, huvuruga uhusiano wao na jamii, hupelekeea kifo (mfano Whitney Houston) n.k. Mienendo mibaya ni mzigo kwa jamii kwa kuwa; jamii inabeba jukumu la kulea wahanga, hupunguza nguvu kazi, hupelekea uvunjifu wa amani n.k

Baadhi ya waathirika wa mienendo hasi hujaribu kujinasua, wachache kati yao hufanikiwa, ila wengi kushindwa kwa kuwa au wao au jamii yao imeshindwa kutoa msaada fasaha. Ikiwa mtu anataka kuondokana na tabia chafu, anapaswa kufanya yafuatayo:

1. Kudhamiria kuacha kama lengo kuu.

Pamoja na kuwa na rundo la malengo ili kufikia maisha bora, mwathirika anapaswa kuamua kuacha tabia chafu kama lengo namba moja. Mtu anapaswa kupanga kwa maandishi siku na saa ya mwisho kufanya jambo hatarishi. Ili kutorudia tena, mtu apange atakachofanya ili kufuta mawazo mabaya.

Inafaa kuacha kidogokidogo (hatua kwa hatua), kusitisha utumiaji wa madawa ya kulevya ghafla kunaweza kusababisha kifo. Mtu anaweza kusoma machapisho juu ya madhara, kushiriki michezo, kujiunga katika vikundi vya watu wema, kuwa karibu na watu sahihi, kuomba ushauri kutoka kwa viongozi wa dini n.k. Malengo yatizame waliofanikiwa kuliko walioshindwa.

2. Kuwazia mafanikio.

Mtu anapaswa kujenga picha ya maisha 'safi'. Kuwaza jinsi atakavyopata ujasiri, jinsi atakavyowekeza nguvu na rasilimali anazotumia kulipia huduma hatarishi. Jinsi mtu husika atakavyokubalika na kuaminika katika jamii, atakavyofaidi utajiri wa jamii yake n.k.

3. Kutafuta njia rahisi na sahihi.

Inafaa kutafuta mbadala wa maisha na ambao ni salama. Hii ikihusisha jinsi ya kuishi na kupata msaada kutoka kwa; ndugu, jamaa, marafiki n.k ambao hawana imani na mwathirika.

Mara nyingi inabidi mtu abadili marafiki, maeneo aliyozoea kukaa (vijiwe), kukataa kusikiliza baadhi ya miziki. Mtu kamwe! asibadili tabia moja dhidi ya nyingine, mfano kunywa pombe kupindukia isiwe mbadala wa kufanya ngono.

4. Kukataa mitizamo hasi

Ili kufanikiwa, mtu anapaswa kukataa mitizamo hasi na misemo kama "kuacha haiwezekani, huu ni ulevi wa kawida, kila mtu ana ulevi wake" n.k. Mitizamo hiyo hasi hufutika kwa kujiambia mara kwa mara "naanza leo na nitapata mafanikio haraka, nitajitahidi kutunza afya yangu, mbona nanii..ameweza, hakuna lisilowezekana" n.k

5. Kujizawadia

Waswahili wanasema "raha jipe mwenyewe babu/ bibi....". Hivyo, ikiwa malengo yamefikiwa kwa kiasi fulani, mtu anapaswa kujipongeza. Zawadi inaweza kugharamiwa kwa fedha zilizokuwa zikitumiwa kulipia huduma angamizi. Mtu anaweza kujipongeza kwa kununua thamani, kutalii, kufanya sherehe na rafiki zake, kusaidia wasiojiweza, kusaidia waathirika wenzake n.k. Kujizawadia huleta uhalisia wa mfanikio ya siku za mbele.

6. Kutafuta msaada,

Watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri husema "tabia ni kama ngozi (haibadiiki), kafiri haachi asili" n.k. Watu wanaotaka na kusababisha mabadiliko husema; tabia hubadilika kulingana na mazingira, utayari wa kuacha na msaada kutoka kwa jamii.

Ili kupata mafanikio ya haraka, mtu anapaswa kuomba ushauri kutoka kwa waliofanikiwa kuacha, wataalamu wa ushauri nasaha, viongozi wa dini, kujiunga na vikundi vya wanaharakati, kuonyesha kwa vitendo dhamira ya kutaka kuacha pamoja na kumshirikisha Mungu.

7. Kuweka rekodi ya mafanikio.

Mtu anapaswa kuweka rekodi kutokana na mafanikio aliyoyapata kutokana na malengo. Kabla ya kulala na kuamka, mtu asome mafanikio ya siku za nyuma. Huku akiweka mikakati juu ya kukabiliana na changamoto za siku kwa siku. Mikakati hiyo iwe ya kawaida na inayotekelezeka kulingana na mazingiza na uwezo wa mtu husika.

8. Kumiliki mihemko.

Watu hupata changamoto kuu siku chache baada ya kuacha iliyokuwa burudani yao. Wengi wao hupata homa, kuarisha, kutapika, kusikia kizunguzungu, kukosa usingizi n.k kwa kuwa wameacha kutumia madawa ya kulevya au pombe kali au sigara.

Bahati nzuri ni kwamba mtu hawezi kufa hususani kama atakula mlo kamili (hususani mboga mboga na matunda) pamoja na maji ya kutosha. Pia mawasiliano ya mara kwa mara kati ya mwathirika na mlezi wake ni muhimu sana. Inapendekezwa mlezi awe ni mtumiaji aliyefanikiwa kuacha.

MCHANGO WA JAMII NI MUHIMU SANA KATIKA KUOKOA WATU WALIOMO HATARINI, WENGI WAO HUTAKA KUACHA LAKINI JAMII HAITAKI. JAMII HAITAKI KWA KUENDELEA KUWABAGUA NA KUTOWAPA USHIRIKIANO.

Monday, February 13, 2012

HOFU KATIKA MAISHA

Hofu au ujasiri ni sehemu ya maisha ya mtu yeyote yule! Kiwango cha hofu au ujasiri hutofautiana kulingana na hisia za mtu. Hisia alizo nazo mtu hutegemea mawazo yake pamoja na mfumo wa kibailojia (homoni).

Hisia hasi za mtu hujengeka kwenye misingi ya woga, ujinga, kutojiamini, n.k. Kwa upande mwingine, hisia chanya hujengeka kwenye misingi ya ufahamu, imani, kujiamini, ujasiri, n.k.

Hofu aliyo nayo mtu yeyote huwa ni mchanganyiko au sehemu mawazo juu ya vitu sita ambavyo ni; kufilisika, kulaumiwa, ugonjwa, kuachwa na mpenzi, uzee na kupoteza maisha.
Mawazo juu vitu hivyo pamoja na suluhu zake ni kama ifuatavyo:

1. Hofu ya kufilisika.

Mtu anaweza kupata hofu ya kupoteza mali alizochuma (hata kupoteza kazi). Hofu hii huwakumba sana watu 'wanaoabudu' mali au hela. Watu hawa hutumia muda wao mwingi kutafuta mali ili kujiimarisha. Watu hawa hutegemea wingi wa mali zao ili kupata amani maishani.

Watu hupata hofu ya kufilisika mara baada ya kuona au kupewa mifano halisi ya watu waliokuwa na mali nyingi na sasa wamefilisika (wamefulia ile mbaya).

Hofu ya kupoteza mali inaweza kuepukwa kwa mtu kukataa kuwa mtumwa wa mali za dunia hii. Mtu anapaswa kuhakikisha anatumia mali na si mali zimtumie yeye. Kila mtu anapaswa kufahamu kwamba mali zake zinaweza kutoweka; kama itatokea awe tayari kuikubali hali hiyo ili aweze kuishinda. Pia ni vizuri kuwa na mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na jamii inayomzunguka mtu

2. Hofu ya kulaumiwa.

Takribani watu wote hufanya au kuhakikisha utekelezaji mambo ili wapate sifa kutoka kwa jamii au kundi fulani la watu. Hivyo, hawajiandai kwa ajili ya kudharauliwa, kutusiwa n.k kutokana na maamuzi au yao au ya kundi. Kuogopa lawama kunawafanya watu waogope nafasi za uongozi, kutoa mawazo yao au kukosoa mambo yasiyo sahihi pale wanapotakiwa kufanya hivyo.

Kuogopa lawama kunaweza kuepukwa kwa kusikiliza na 'KUTATAA' yale mtu anayoambiwa juu ya ugumu wa jambo fulani. Mtu anapaswa kuamini mawazo aliyopewa na watu sahihi na anayotekeleza kulingana na hali yatampa tuzo.

Pia mtu afahamu watu wanaomkosoa wana; lengo gani, elimu, au uzoefu gani juu ya jambo husika, kama wanalenga kujenga au kubomoa n.k. Ikiwa watu wangeogopa lawana wasingefanya mambo ya maana kwao au kwa jamii zao. Lawama ni miongoni mwa mavuno, na lawama hazikwepeki.

3. Hofu ya ugonjwa.

Kuna nyakati fulani watu hupata hofu juu ya afya zao. Watu hupata hofu ya homa fulani kwa sababu ya kutokuwa na elimu juu ya ugonjwa, kuona watu walioathirika na ugonjwa fulani, kutofuata kanuni za afya wakati wa kufanya jambo fulani(mfano kushiriki ngono isiyo salama) n.k. Mtu anaweza kupatwa na mafua akahisi ana Kifua Kikuu, UKIMWI.....

Hofu ya homa au ugonjwa fulani inaweza kuondolewa kwa kutafuta habari sahihi za ugonjwa husika, kupata ushauri, kupima, kufuata kanuni bora za maisha kama; mapenzi salama, kunywa maji safi na salama, kufanya mazoezi ya viungo, kula mlo kamili n.k

4. Hofu ya kupoteza penzi.

Mtu anaweza kupata hofu juu ya mwenendo wa kimapenzi wa mpenzi wake baada ya kuambiwa maasi ya kimapenzi yanaoyafanywa na marafiki wa mpenzi wake, kusimuliwa mikasa ya kimapenzi, kuhisi kama anasalitiwa na mpenzi wake n.k. Hofu ya kupoteza penzi kumfanya mtu aamini mapenzi yananunuliwa au kuchukia jinsia nyingine.

Ili kuepuka hofu ya kupigwa chini, mtu anapaswa kuwa karibu na mpenzi wake ili apate kujua ukweli wa mambo, kukumbuka mambo mazuri aliyoyafanya na mpenzi wake, kuchuja anachoambiwa na marafiki zake kuhusu mpenzi wake n.k. Mtu anapaswa kuamini penzi halipotei; kwani penzi ni muendelezo usioisha wa hisia baina ya mtoaji na mpokeaji. Kuaminiana ni suluhu kuu ya hofu ya kupoteza penzi.

5. Hofu ya uzee.

Watoto wadogo hupenda kukua na kuitwa watu wazima. Watu wazima hukataa utu uzima na ambao ni lazima kwa viumbe hai wote. Watu huogopa uzee kwa kuwa wanaihisi watapoteza mvuto, watapitwa na 'wakati', kuzeeka kutawafanya kutofurahia maisha, kupatwa magonjwa ya uzeeni n.k

Kutokana na hofu ya kuzeeka, baadhi ya watu hupenda kuvaa, kuongea, kutumia vipodozi vya ngozi na nywele ili waonekane ni vijana. Baadhi ya watu hupenda kujihusisha na makundi ya vijana; na kuwaacha watu wa umri wao.

Ili kuepuka hofu ya kuzeeka, mtu anapswa kujua ya kwamba kuwa na umri mkubwa katika jamii ni hazina, ni dalili ya kukua, watu wazima huwa na busara na hekima kwa ajili ya kulea jamii (vijana) kwa kuwa mienendo yao bora na ya kuigwa. Uzee ni tunu kutoka kwa Mungu.

6. Hofu ya kupoteza maisha.

Baadhi ya watu hupata hofu ya kupoteza maisha baada ya: kuona mwili au jeneza la marehemu, kuona kaburi, kuugua kwa muda mrefu, kuwaza juu ya kufa. Watu wengine hupata hofu ya kufa baada ya kukata tamaa ya maisha, kukosa kazi, kukosa watu wa kuwalea, kutengwa na jamii, rafiki zao (hasa wa utotoni) kufariki, kusikia magonjwa ya ajabu na yasiyo na tiba yakiua watu wengi n.k

Hofu ya kupoteza maisha huwafanya baadhi ya watu kutotia bidii katika shughuli za uzalishaji mali, kuuza mali walizochuma au kufuja mali zao hatimaye wao au jamii inayowategemea huingia kwenye dimbwi la umasikini wa kupindukia.

Ili kuepuka hofu ya kufa, mtu anapswa kujua kufa ni sifa ya viumbe hai vyote; hata Yesu, Musa na manabii maarufu walikufa. Pia mtu anapokufa hubaki akitukuzwa kwa yale mema aliyosema na kutenda, kwa msimamo wake katika kuleta mabadiliko kwa familia au jamii yake. Mali alizochuma mtu wakati wa uhai wake zitawakilisha uwepo wake hapa duniani.
HOFU ZOTE NI HISIA ZA AKILI, IKIWA MTU ATAZIENDEKEZA ATAANGAMIA!!!...

Monday, February 6, 2012

HUJUMA AFANYAZO MTU DHIDI YA NAFSI YAKE

Maria Robinson: "Hakuna mtu yeyote anayeweza kurudisha muda nyuma au kufuta historia ili aanze upya, ila mtu yeyote anaweza kuanza leo na kuandika ukurasa mpya wa mafanikio". Mtu yeyote anaweza kuanza mchakato wa kuboresha maisha yake wakati wowote ule, kama tu AKIDHAMIRIA kufanya hivyo.
Kwa bahati mbaya, watu huanza harakati za kupambana na maisha duni huku "wakikumbatia hujuma" dhidi ya nafsi zao. Hujuma hizo ni kama zifuztazo:

1. Kujihusisha na mtu au watu wasiosahihi.

Maisha ni mafupi sana, hususani ikiwa mtu anatumiwa kumnufaisha mwingine. Ikiwa mtu anahitaji msaada, atajenga mazingira ya kupata msaada. Watu wasiosahihi (wanyonyaji) hujenga mazingira ya kuwatumia wanyonge (maskini) ili kujinufaisha.

Watu hawa hujenga au kuimarisha uhusiani wakiamini tu! watapata msaada ili watimize malengo yao, huwatumia wanyonge kama ngazi, (mfano kuwapa msahara duni, kuwatumikisha zaidi ya uwezo n.k) bila kujali mustakabali wa afya n.k wa wanaowatumia. Mabosi hawa hawapo tayari kutoa msaada wa hali au mali ili kuwakwamua wafanyakazi wao.

Kwa hahati mabaya au kwa kujua au kwa kutojijua vibarua "huwaabudu mabosi hawa wanyonyaji na ambao huwatelekeza pindi wanapozeeka au kupata matatizo makubwa ya kiafya. Hatimaye vibarua huishia kuishi kama ombaomba wa kutupwa.

2. Kukimbia changamoto.

Ni vigumu sana mtu kukwepa changamoto zote zinazomkabili. Hivyo mtu anapaswa kusimama imara dhidi ya dhoruba za kimaisha. Watu hufanikiwa kwa kupitia changamoto moto moto. Kufanikiwa huwa ni matunda ya kukubali, kujifunza na kutatua changamoto zinazowakabili wakati wa kipindi chake chote cha maisha yao.

Watu hufanya hujuma dhidi ya nafsi au jamii kwa kukimbia changamoto bila ya kujua ya kwamba, changamoto zipo kwa ajili ya watu na watu ndio wao au bila ya kujiuliza, je watakimbia changamoto ngapi ili wafanikiwe?

3. Kujidanganya.

Mtu anaweza kumdanganya yeyote kaika dunia hii, lakini hawezi kujidanganya yeye mwenyewe. Maisha ya mtu huimarika pale anagundua na kuchangamkia fursa. Moja ya kitu kigumu ni kuukubali ukweli, ukweli ambao ni mlima ambao mtu anapaswa kuupanda ili afikie 'kilele' cha mafanikio.

Watu husaidiwa na mazingira au wale wanaowazunguka ili kujidanganya. Baadhi ya watu hujidanganya wana maisha mazuri ili hali hawajui au hawajapanga kesho au kesho kutwa yake itakuwaje, hawajafanya jitihada zozote kujikwamua.

4. Kujirudisha nyuma.

Baadhi ya watu (watu walio wengi) hawapo tayari kusimama mstari wa mbele huku wakipigania haki zao, hawapo tayari kusimama imara wakati wa kuwasilisha na kufafanua madai yao; huwaachia wawakilishi ambao si wahanga kupeleka hoja na kuwatetea (hata kwa mambo wanayoweza kuyafafanua wao wenyewe), wao hukaa na kusubiri taarifa za msuguano kutoka wa wanyonyaji kupitia wawakilishi.

Kwa bahati mbaya zaidi, baadhi ya watu huridhia haki zao zinyakuliwe wakiamini Mungu ndiye mtoaji. Kila mpiganaji anapaswa kuwa na roho ya kibinadamu, lakini asijishushie hadhi kwa kujiweka 'mkiani' au kijidharau.

5. Kufuata mkumbo.

Moja ya changamoto zinazomkabili mtu popote pale anapoishi ni kutaka kuishi maisha yake, maisha yasiyo na ushawishi kutoka kwa kundi fulani la watu katika jamii.
Kutokana na changamoto hiyo, watu hujikuta wakijidhulumu kwa kuiga maisha (kufuata mkumbo) ya watu waliofanikiwa wakiamini nao watafanikiwa au ili wapate kukubalika.

Watu wa ukweli ni wale wanaoweka vigezo vyao, kwa kuzingatia uwezo wao; vigezo wanavyoamini vitawatoa kimaisha. Vigezo au vipaumbele vitakavyowafanya wawe maarufu kwa mali, maelewano, mahusiano na jamii yao; si kwa mawazi, kuhudhuria klabu au vipodozi n.k

6. Kuogopa makosa.

Kufanya kitu bila ya kufanikiwa (kwa makosa) hata mara mia ni bora kuliko kutofanya chochote. Kila aliyefanikiwa ameanguka mara nyingi, na kila anguko limenfanya mtu aimarike zaidi. Baada ya kufanya jitihada za bila matunda yanayoridhisha, mtu hufanikiwa.

Kwa mfano, mwanasayansi aliyegundua balbu ya umeme alifanya majaribio mara 3000 na hatimaye akafanikiwa kutengeneza balbu inayowaka. Hata alipotakiwa na wanahabari kueleza palipokuwa panamshinda hivyo kufanya majaribio mengi aliwaambia "sijui tatizo lilikuwa ni nini".

7. Kununua furaha.

Watu hujidanganya ya kwamba wakimiliki kitu/ vitu fulani vya thamani au kujihusisha na mtu/ watu fulani watakuwa na furaha maishani. Hivyo, hutumia muda nwingi au rasilimali zao kugharamia furaha. Baadhi ya watu hudiriki kununua baadhi ya bidhaa za gharama, kugharamia mitoko na watu maarufu au kutafuta mahusiano ya kimapenzi na watu maarufu ili furaha yao itimie. Mwishowe hupata mgogoro wa nafsi na si furaha.

Ukweli ni kwamba, vitu vya kawaida ndivyo vinavyoleta furaha ya kweli na ya kudumu; vitu au mambo anayafanya mtu kwa hiari ya moyo na akili yake; vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wa mtu.

8. Kutoishughulisha akili.

Mtu asiyefikiri kwa ufasaha ndiye anayetekwa au kutumiwa na shetani kutekeleza uovu. Kila mtu anapaswa kuchambua kwa kina hali aliyonayo na kuchukua hatua sahihi.

Mtu anapaswa kuitumikisha akili ili kupata ya mambo aliyowahi kuambiwa hayawezekani. Kusonga mbele ni kukubali kukabili hatari. Pia mtu asiwaze (asiwaze bila mapumziko) kiasi cha kupata msongo mawazo.

9. Kuamini ukamilifu.

Wapiganaji hawaamini wamefanikiwa kwa 100% hata wapate fursa nzuri kiasi gani! Baadhi ya watu hubweteka kwa mafanikio kidogo, wakiamini wamefikia kilele, wengine huridhia kuacha kazi zao za ziada. Mabilionea hulazimishwa na mafanikio kufanya kazi zaidi; huku wakiamini mafanikio waliopata ndio mwanzo tu, na wanapaswa kutafuta fursa bora zaidi.
AMUA KUACHA HUJUMA LEO!